MUUAJI SUGU HATIMAYE AKAMATWA WILAYANI SENGEREMA Mtu mmoja anayesadikiwa kufanya mauaji ya watu mbalimbali katika Wilaya ya Sengerema amekamatwa usiku wa kuamkia leo katika kata ya Nyatukala wilayani hapa. Mtuhumiwa huyo amejulikana kwa majina Gelvas Mathias (22) mkazi wa Nyatukala wilayani Sengerema ambapo amekiri kufanya mauaji hayo na kudai kuwa ametenda matukio hayo kwa kushirikiana na watu wengine. Mtuhumiwa huyo licha ya kukiri kufanya mauaji hayo pia anatuhumiwa kuwa amekuwa akiiba vitu mbalimbali na kwenda kuwekeza kwa mtu kisha kuwauzia watu mbalimbali vitu vya wizi. Mtemi wa Jeshi la Jadi maarufu kama sungusungu wa eneo hilo bwn Nsiya ntemi akitoa taarifa kwa Jeshi la polisi wilaya ya Sengerema baada ya kufika eneo la tukio amewashukuru wananchi kwa kutokujichukulia sheria mkononi. Hata hivyo Jeshi la polisi limeondoka na mtuhumiwa huyo na huku likiwaomba wananchi kutoa taarifa kwa jeshi hilo mara wanapomtilia shaka mtu katika maeneo yao.
Posts
Showing posts from August, 2017
- Get link
- X
- Other Apps
TATIZO LA KUANGUKA GHAFLA LAWAKUMBA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI LWENGE WILAYANI SENGEREMA Hali ya taharuki imetanda katika shule ya MSingi Lwenge Wilayani Sengerema baada ya takribani wanafunzi sita kukumbwa na tatizo la kuanguka ghafla shuleni hapo. Mwenyekiti wa kitongoji cha Lwenge Bwn ,Deus Masunzu amethitisha kutokea kwa tukio hilo . Kwa upande wake Afisa elimu shule za msingi Wilayani Sengerema Osicar Kapinga amesema kuwa tukio hilo lisihusishwe kamwe na imani za kishirikina kwani ni suala la kisaikolojia. Na Peter Marlesa.
- Get link
- X
- Other Apps
KAMATA KAMATA YA BODABODA YAZUA TAHARUKI WILAYANI SENGEREMA Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wilayani Sengerema mkoani Mwanza wamelitupia lawama jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wilayani Sengerema kwa kile kinachodaiwa linashirikiana na kamanda wa waeendesha pikipiki kuwakamata bila kufuata utaratibu na pikipiki zao kupelekwa sehemu isiyo rasimi hali iliyozua sintofahamu kwa madereva hao. Waendesha bodaboda hao wamedai kuwa kumekuwa wakikamatwa bila kufuata utaratibu uliowekwa hali iliyowalazimu kuitisha mkutano na viongozi wa umoja waendesha pikipiki ngazi ya mkoa kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa kero hiyo. Kufuatia sakata hilo Radio sengerema imemtamtafuta Mratibu wa Elimu kwa umma kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Sengerema Coplo Echika Mbozi ili kutolea ufafanuzi suala hilo la kukamatwa waeendesha pikipiki ambapo amekana madai hayo na kusema kuwa wanaolalamika ni watu ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani. Malalamiko y
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI aeleza walivyochunguza moyo wa Manji Daktari katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu namna walivyouchunguza moyo wa mfanyabiashara Yusuf Manji. Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohammed Janabi (51) ametoa ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Manji. Profesa Janabi ameieleza Mahakama jinsi walivyoangalia vyuma vilivyopo kwenye moyo wa Manji kama vimeziba au la. Akiwa shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi, Profesa Janabi aliongozwa na wakili Hajra Mungula kutoa ushahidi mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha. Manji ambaye katika hati ya mashtaka jina lake ni Yusufali Manji, alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16 akidaiwa kati ya Februari 6 na 9 katika eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
- Get link
- X
- Other Apps
MBICHI NA MBIVU ZA KUPINGA USHINDI WA KENYATTA HADHARANI IJUMAA Majaji wa Mahakama ya Juu wameanza kuandika uamuzi wa kesi ya kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta, iliyowasilishwa na kiongozi wa Muungano wa upinzani NASA Raila Odinga. Hatua hii inakuja baada ya Majaji hao kutamatisha kibarua cha kusikiliza Mawakili wa upande wa Tume ya uchaguzi, wale wanaomwakilisha rais Kenyatta na wale wa muungano wa upinzani NASA. Mawakili wa NASA, wakiongozwa na James Orengo, wanataka Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo baada ya kuonesha kuwa kulikuwa na ushahidi mkubwa, Uchaguzi huo haukuwa huru na haki. Akitoa ripoti ya mwisho, Orengo alisema ikiwa Mahakama hiyo itaangalia kikamilifu ushahidi wote uliowasilishwa, basi ushindi huo utatupiliwa mbali. Paul Muite anayewakilisha Tume ya Uchaguzi katika kesi hiyo alisema kuwa, pamoja na kwamba huenda kulikuwa na dosaro ndogondogo, zoezi hilo lilikwenda vizuri. Pande zote mbili, upinzani NASA na Tume ya Uchaguzi i
- Get link
- X
- Other Apps
NYAVU HARAMU ZAWAPONZA WATU SITA WILAYANI SENGEREMA Watu sita wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya sengerema mkoani mwanza kwa tuhuma ya makosa mawili ya kupatikana na nyavu haramu. Akisoma shitaka linalowakabili mbele ya hakimu wa mahakama hiyo BI Monica Ndyekobora .mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Inspecta Slivesta Mwaiseje,amewataja washitakiwa kuwa ni Kampichi Salvatory mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa nyakaliro, Simeo Raphael mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Nyakaliro,Salvatory Mkwesa mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa Isenyi, Venancy Masana mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa Isenyi, na Fransisco Nicas mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa L umeya . Inspecta Mwaiseje ,amesema kuwa kosa la kwanza washitakiwa wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa kosa la kupatikana na nyavu haramu kinyume na kifungu namba 66 ki
- Get link
- X
- Other Apps
WATAKAOKAIDI KUJENGA CHOO KUBURUZWA MAHAKAMANI WILAYANI SENGEREMA Kamati ya mazingira ya Kata Ibisabageni Wilayani Sengerema imetangaza vita kali kwa wananchi wanaokaidi kujenga vyoo katika makazi yao kwa kuwa hali hiyo inaweza kusababisha magonjwa ya milipuko katika siku za usoni . Kauli hiyo imetolewa mjumbe wa kamati ya mazingira ya kata hiyo Bi,Martha Buta na mhasibu wa kamati hiyo Bi . Emeryciana Patrick ambapo wamesema kuwa baadhi ya wananchi hawajajenga vyoo katika makazi yao wakisubili kusukwa na serikali ili hali ni wajibu wao kufanya hivyo. Nae katibu wa mazingira wa kata ya Ibisabageni Bwn,Paschael Ng’ombeyapi amesema kuwa kwa wale wanaokaidi kujenga vyoo katika makazi yao watachukuliwa hatua kali za kisheria huku akiwaomba wananchi kushirikiana kutunza mazingira . Kuhusuana na suala la upandaji miti Bwn, Ng’ombeyapi amewataka wananchi kupanda miti katika meneo yao ili kutunza mazingira pindi msimu wa mvua utaka
- Get link
- X
- Other Apps
MWILI WA ASKARI POLISI WAKUTWA UKIELEA NDANI YA ZIWA VICTORIA MANISPAA YA BUKOBA Askari polisi wa kitengo cha Intelijensia katika mkoa wa Kagera aliyefahamika kwa jina la Mussa Salum Musanya amekutwa amefariki baada ya mwili wake kuokotwa ukielea kwenye ufukwe wa ziwa Victoria katika eneo la Kiroyera manispaa ya Bukoba. Askari huyo wa polisi ambaye ameopelewa kwenye maji huku mwili wake ukiwa na sare za jeshi la polisi alitoweka nyumbani kwake na kupotea katika mazingira ya kutatanisha siku tatu zilizopita na kila walipomtafuta hakuweza kupatikana mpaka mwili wake ulipokutwa ukielea kwenye fukwe ya ziwa Victoria. Na Veronica Martine
- Get link
- X
- Other Apps
DIWANI ASHAMBULIWA KWA KUKATWA KATWA NA MAPANGA WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA Diwani wa Kata ya Nyakahanga wilayani Ngara mkoani Kagera, Charles Bechumila ameshambuliwa kwa kuchomwa mishale ikiwa ni pamoja na kukatwa na panga na watu wasiofahamika alipokuwa kwenye ziara. Kiongozi huyo anadaiwa alishambuliwa na watu wasiojulikana mapema leo alipokuwa kwenye msafara wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mhe. Godfrey Mheluka uliokuwa katika operesheni ya kuwaondoa watu wanaodaiwa kuvamia maeneo ya wafugaji katika Kijiji cha Kashanda. Katika shambulizi hilo lililotokea leo Agosti 29 asubuhi, diwani wa Nyakahanga, Charles Bechumila amejeruhiwa na amepelekwa katika Hospitali Teule ya Nyakahanga. Afisa Tarafa ya Bugene Nyaishozi, Rozaria Christian amesema walikuwa kwenye operesheni halali na wakulima hawakuwa na taarifa hivyo baada ya kuwakamata wawili ndipo kundi la watu lilijitokeza likionyesha kuwa lilijiandaa kuwashambulia. Aidha Christian amefafanua kwamba watu kad
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS MAGUFULI KUUNGURUMA MKUTANO WA ALART Rais John Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa 33 wa kawaida wa Jumuia ya Tawala za Mitaa (Alat). Mwenyekiti wa Alat, Gulamhafeez Mukadam amesema, awali mkutano huo ulipangwa kufanyika Septemba 19 hadi 22 lakini kutokana na baadhi ya wanachama kutokusanya fedha kwa wakati, umesogezwa na sasa utafanyika Oktoba 2 hadi 5 mkoani Mbeya. Amesema kutokana na mamlaka za Serikali za mitaa kuwa wanachama wa Alat na Rais ndiye mwenye dhamana na Serikali za Mitaa, hivyo atakuwa mgeni rasmi katika mkutano huo. Amesema pamoja na mambo mengine, mkutano huo ni fursa ya kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali Kuu na za mitaa kwa ajili ya kutoa maelekezo na miongozo ya kisera kwa watekelezaji ambao ni mamlaka ya serikali za mitaa nchini. Mukadam amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi kwenye mamlaka ya Serikali za Mitaa ni chachu ya maendeleo, halmashauri zitenge ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vidogovidogo na vikub
- Get link
- X
- Other Apps
WANANCHI WANUFAIKA KUPITIA KILIMO CHA MUHOGO WILAYANI SENGEREMA. Imeelezwa kuwa wananchi wameonyesha mwamko wa kulima zao la muhogo kutokana na zao hilo kuwa la kibiashara katika wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza. Hayo yamesemwa na wananchi wa kijiji cha Kijuka ambapo wameelezea zao la muhogo limekuwa zao la biashara kutokana na kupewa elimu na maafisa kilimo ngazi ya kata na wilaya hali iliyowalazimu kujikita katika kulima zao hilo la muhogo. Clip wananchi………….. Kwa upande wake Afisa kilimo wilaya ya Sengerema SAIMON BUTELA amesema zao la muhogo ni kati ya mazao ambayo yanastahimili ukame hivyo wakulima wanashauriwa kulima zao hilo ili wajiinue kiuchumi. Clip afisa kilimo 1……………. Pia zao la muhogo ni zao la chakula na biashara hivyo wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima ili waendelee kulima kilimo hicho. Clip afisa kilimo 2………. Aidha Bwn, Butera amewaomba maafisa ugani wa kila kata kujipanga kuanza kutoa elimu kwa wakulima wao ili waweze kunufaika kilimo n
- Get link
- X
- Other Apps
UHUJUMU UCHUMI WAWAFIKISHA MAHAKAMA YA WILAYA YA SENGEREMA WATU WATANO. Watu watano wamefikishwa katikas mahakama ya wilaya ya sengerema mkoani mwanza kwa tuhuma ya kuingilia huduma ya msingi ya kuhujumu uchumi. Akisoma shitaka linalowakabili mbele ya hakimu n wa mahakama hiyo BI Monica Ndyekobora . mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Inspecta Slyvesta Mwaiseje ,amewataja washitakiwa kuwa ni Andrew Fredinand ,mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Kasalula Ukerewe, Arafa Wanjala mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Bukongo Ukerewe ,Ephrahimu Kusekwa mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa Kisesa magu , Masinde Cosmas mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Katunguru, na Slyvester Elias mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Katunguru . Inspecta Mwaiseje ,amesema kuwa washitakiwa wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa kosa la kuingilia huduma za msingi kinyume
- Get link
- X
- Other Apps
WAKAZI WA KATA YA IBONDO WILAYANI SENGEREMA WAJITOLEA KUCHIMBA MTARO WA MAJI Diwani wa kata ya Ibondo Wilayani Sengerema Mathias Mashauri kwa kushirikiana na wananchi wa kata yake wameamua kuchimba bomba la maji ili kupata huduma ya maji katika kata hiyo kutokana na adha ya uhaba wa maji inayowakabili kwa muda mrefu. Hayo yamebainika wakati jitihada hizo za kuchimba bomba la maji zikiendelea, diwani huyo amesema kuwa lengo la kuwahamasisha wananchi wake ni kuondoa changamoto ya maji iliyokuwa inawakabili wananchi hao kwa muda mrefu. Hata hivyo Mh,Diwani ameipongeza serikali kwa kuleta maji ya bomba katika kata hiyo hali iliyowasaidia wananchi Nao wananchi wa kijiji hicho wameelezea namna hali ya maji inavyowasibu katika kijiji hicho.
- Get link
- X
- Other Apps
WILAYA YA SENGEREMA YAKABILIWA NA UKOSEFU WA SHULE Afisa tawala wa wilaya ya sengerema bwana ,ARONI LAIZER amewapongeza wananchi wa kijiji cha ILEKANILO kata ya KASUNGAMILE kwa juhudi za kujitolea kujenga shule ya msingi ya Bulyangele katika kijiji hicho. Pongezi hizo amezitoa wakati wa harambee ya kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ambaye pia, alikuwa mgeni rasimi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Emmanuel Kipole na kusema kuwa wananchi wa kijiji hicho wameonesha nia njema kwani hana budi kuwashukuru. Pia mgeni rasimi huyo ameunga mkono juhudi za wananchi hao kwa kutoa mifuko ishirini na moja ya saruji itakayowasaidia kukamilisha ujenzi wa shule ya Msingi Bulyangele. Nae Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh WILLIAM MGANGA NGELEJA amewaunga mkono wananchi hao kwa kutuma mwakilishi wake na kuchangia mabati mia moja ili kuezeka majengo yaliyobaki katika shule hiyo. Sanjari na hayo Jumla ya shilingi milioni tano na elfu arobaini na
- Get link
- X
- Other Apps
KUNI ZA SABABISHA WANANCHI KULALAMIKA Wananchi wa kijiji cha Ikoni kata ya Buzilasoga Wilayani Sengerema ,wamemtupia lawama mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikoni Evaline Mkando kwa kuwaagiza wanafunzi kuni pamoja na maji hali ambayo imeleta sintofahamu kwa wazazi. Wananchi hao wametoa malalamiko hayo kwa mbunge wa jimbo la Sengerema Mh,William Mganga Ngeleja alipotembelea kijiji hicho ambapo wamedai mwalimu huyo amekuwa akiwaagiza watoto kuni pamoja na maji hali iliyowalazimu wazazi kuhoji kuni hizo zinafanya kazi gani shuleni hapo. Akijibu malalamiko hayo ya wananchi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikoni EVALINE MKANDO amesema katika shule yao kuna utaratibu ambao wanaufanya wa kuwaagiza wanafunzi kuni kwa ajili ya kupikia chakula wakati wa mitihani. Aidha Mwalimu mkuu huyo amesema maji hayo hutumika kuwasaidia wanafunzi kufanya usafi wa madarasa kwa kuwa madarasa hayana sakafu. Na Deborah Maisa.
- Get link
- X
- Other Apps
UKOSEFU WA SHULE YA MSINGI WAGEUKA KAA LA MOTO MKOANI GEITA Kitongoji cha Bungwe kijiji cha Nyaseke kata ya Bulela chenye mkoani Geita zaidi ya kaya 120 kinakabiliwa na ukosefu wa shule ya msingi hali inayopelekea wananchi kuchanga fedha kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja cha kujenga shule. Akiongea na Radio Sengerema mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw,Mahesa .L.Mahesa amesema kwa sasa tayari wamenunua kiwanja zaidi ya hekari mbili kwa ajili ya ujenzi wa shule . Kwa upande wao wananchi wamesema kutokana na kukosa shule katika kitongoji hicho watoto wanatembea umbali mrefu kufuata huduma ya Elimu na kudai kuwa watoto wao kipindi cha mvua wanashindwa kuhudhuria masomo kutokana na kutembea umbali mrefu bila ya kuwa na usafiri wowote. Pamoja na hayo wameiomba serikali pamoja na wadau wa Elimu kuwasaidia ujenzi wa shule ambapo kwa sasa wamesomba mawe kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa msingi kwa nguvu za wananchi.
- Get link
- X
- Other Apps
WATAKAO UZA VIWANJA KINYEMELA KUKIONA CHA MOTO Uongozi wa kata ya Nyamizeze Wilayani Sengerema umetangaza kiama kwa Wananchi wa kata hiyo wanaouza na kununua viwanja vya makazi kinyemela kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria . Kauli hiyo imetolewa na afisa mtendaji wa kata ya Nyamizeze Bi.Mariam Simon kufuatia mwanaume mmoja kuuza kiwanja cha famailia yake kinyemela wakati mama wa familia na watoto wake tisa wakiwa shambani katika shughuli za kilimo hali iliyopelekea kuanza kulala nje bila msaada wowote. Bi.Mariam amesema kuwa wananchi wakihitaji kuuza ama kununua kiwanja hawanabudi kupitia taratibu zote ili kuwa na hati miliki ya viwanja hivyo ili kuepuka kusababisha migogoro katika jamii. Katika hatua nyingine afisa huyo mtendaji wa kata ya Nyamizeze amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa viongozi husika pindi wanapobaini mtu yeyote ameuza ama kununua kiwanja kinyemela ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake . Na Emmanue
- Get link
- X
- Other Apps
MAMA ALALA NJE BAADA YA KUUZWA KINYEMELA KIWANJA CHA MAKAZI . Mama mwenye watoto tisa amelazimika kulala nje kwa muda mrefu , baada ya baba wa familia kumtumia rafiki yake kuuza kiwanja cha familia yake kinyemela na kutokomea kusikojulikana wakati mama wa familia na watoto wakiwa shambani kwa shughuli za kilimo katika kitongoji cha Iseni kata ya Nyamizeze Wilayani Sengerema. Radio Sengerema imefika katika eneo la familia hiyo ya Bwn Jumanne Sabuni linalodaiwa kuuzwa na kuzungumza na mama wa familia hiyo Bi, Lucia Kazila ambapo ameeleza kuwa akiwa shambani alikuta kiwanja hicho kimeuzwa bila kupewa taarifa na mme wake na kuanza kulala nje mpaka sasa. Philipo Mathias ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Iseni amekiri kuuzwa kwa eneo hilo kinyemela huku akidai kuwa kwa sasa anaendelea kufanyajitihada ili mama huyo apate hifadhi . Nae afisa mtendaji wa kata ya Nyamizeze Bi. Mariam Simon akikiri kupokea taarifa za
- Get link
- X
- Other Apps
DC AWANYOOSHEA KIDOLE WAKURUGENZI WATAKAOSHINDWA KUSIMAMIA MAENDELEO YA WANAFUNZI Mkuu wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Mh,Emmanuel Kipole amewataka wakurugezi watendaji wa halimashauri ya Sengerema na Buchosa pamoja na maafisa elimu kutoa taarifa ya maendeleo ya wanafunzi. Hayo ameyasema katika baraza la madiwani wa halmashauri ya Buchosa ambapo mbunge wa jimbo la Buchosa ambaye pia ni waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mh, Dkt.Charles Tizeba alipotaka kujua kama suala la utoro linafahamika kwenye Ofisi ya mkurugenzi kwani katika shule ya Sekondari Lugata utoro umekithiri. Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh, Kipole amesema kumekuwepo na changamoto hiyo ya utoro na wataalamu wa idara hiyo hawatoi taarifa ya maendeleo katika idara zao. Aidha Mkuu wa wilaya amewata wazazi kushirikiana na walimu katika kuhakikisha maendeleo ya wanafunzi,huku akitoa taarifa kuhusu kupanuliwa kwa shule ya sekondari nyehunge na kwamba mwaka huu itapokea w