UKOSEFU  WA SHULE YA MSINGI WAGEUKA KAA LA MOTO MKOANI GEITA
Related image

Kitongoji cha Bungwe  kijiji cha Nyaseke kata ya Bulela chenye  mkoani Geita zaidi ya kaya 120 kinakabiliwa na ukosefu wa shule ya msingi hali inayopelekea wananchi kuchanga fedha kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja cha kujenga shule.

Akiongea na Radio Sengerema mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw,Mahesa .L.Mahesa amesema kwa sasa tayari wamenunua kiwanja  zaidi ya hekari mbili kwa ajili ya ujenzi wa shule .

Kwa upande wao wananchi wamesema kutokana na kukosa shule katika kitongoji hicho watoto wanatembea umbali mrefu kufuata huduma ya Elimu na kudai kuwa watoto wao kipindi cha mvua wanashindwa kuhudhuria masomo kutokana na kutembea umbali mrefu bila ya kuwa na usafiri wowote.


Pamoja na hayo wameiomba serikali pamoja na wadau wa Elimu kuwasaidia ujenzi wa shule ambapo kwa sasa wamesomba mawe kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa msingi kwa nguvu za wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA