WATAKAO UZA VIWANJA KINYEMELA KUKIONA CHA MOTO
Uongozi wa kata
ya Nyamizeze Wilayani Sengerema umetangaza
kiama kwa Wananchi wa kata hiyo
wanaouza na kununua viwanja
vya makazi kinyemela
kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria .
Kauli hiyo imetolewa na afisa mtendaji wa kata ya
Nyamizeze Bi.Mariam Simon kufuatia
mwanaume mmoja kuuza kiwanja cha
famailia yake kinyemela wakati mama wa
familia na watoto wake tisa wakiwa shambani katika shughuli za kilimo hali iliyopelekea kuanza kulala nje bila msaada wowote.
Bi.Mariam amesema kuwa
wananchi wakihitaji kuuza ama kununua kiwanja hawanabudi kupitia
taratibu zote ili kuwa na hati miliki
ya viwanja hivyo ili kuepuka kusababisha
migogoro katika jamii.
Katika hatua nyingine afisa huyo mtendaji wa kata ya
Nyamizeze amewaomba wananchi kutoa
taarifa kwa viongozi husika pindi wanapobaini
mtu yeyote ameuza ama kununua kiwanja kinyemela ili hatua kali za kisheria
zichukuliwe dhidi yake .
Na Emmanuel Twimanye.
Comments
Post a Comment