MBICHI NA MBIVU ZA KUPINGA USHINDI WA KENYATTA
HADHARANI IJUMAA
Majaji wa Mahakama ya Juu wameanza kuandika uamuzi wa
kesi ya kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta, iliyowasilishwa na kiongozi wa
Muungano wa upinzani NASA Raila Odinga.
Hatua hii inakuja baada ya Majaji hao kutamatisha
kibarua cha kusikiliza Mawakili wa upande wa Tume ya uchaguzi, wale
wanaomwakilisha rais Kenyatta na wale wa muungano wa upinzani NASA.
Mawakili wa NASA, wakiongozwa na James Orengo,
wanataka Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo baada ya kuonesha kuwa
kulikuwa na ushahidi mkubwa, Uchaguzi huo haukuwa huru na haki.
Akitoa ripoti ya mwisho, Orengo alisema ikiwa Mahakama hiyo
itaangalia kikamilifu ushahidi wote uliowasilishwa, basi
ushindi huo utatupiliwa mbali.
Paul Muite anayewakilisha Tume ya Uchaguzi katika kesi
hiyo alisema kuwa, pamoja na kwamba huenda kulikuwa na dosaro ndogondogo, zoezi
hilo lilikwenda vizuri.
Pande zote mbili, upinzani NASA na Tume ya Uchaguzi
iliwasilisha ripoti mbili tofauti zikionesha taarIfa zilizopatikana ndani ya
fomu za kujumuisha matokeo lakini pia mitambo ya kuhifadhi matokeo.
Comments
Post a Comment