UHUJUMU UCHUMI
WAWAFIKISHA MAHAKAMA YA WILAYA YA SENGEREMA WATU WATANO.
Watu watano
wamefikishwa katikas mahakama
ya wilaya ya
sengerema mkoani mwanza
kwa tuhuma ya
kuingilia huduma ya
msingi ya kuhujumu uchumi.
Akisoma shitaka
linalowakabili mbele ya hakimu
n wa
mahakama hiyo BI Monica
Ndyekobora .mwendesha
mashitaka wa jeshi
la polisi Inspecta Slyvesta
Mwaiseje,amewataja
washitakiwa kuwa ni Andrew
Fredinand ,mwenye umri wa
miaka 20 mkazi
wa Kasalula Ukerewe,Arafa Wanjala
mwenye umri wa
miaka 19 mkazi wa
Bukongo Ukerewe,Ephrahimu Kusekwa
mwenye
umri wa miaka
36 mkazi wa Kisesa
magu ,Masinde Cosmas mwenye
umri wa miaka 32
mkazi wa Katunguru, na
Slyvester Elias
mwenye umri wa
miaka 26 mkazi wa
Katunguru .
Inspecta Mwaiseje ,amesema
kuwa washitakiwa wote
kwa pamoja wanashitakiwa kwa
kosa la kuingilia
huduma za msingi
kinyume na kifungu
namba 57 kifungu kidogo
cha 1 cha
uhujumu uchumi sura
ya 200 inasomwa
pamoja na aya
ya kumi na
moja ya jeddwali
la kwanza la
sheria na kifungu
namba 60 kifungu
kidogo cha pili cha
sheria ya uhujumu
uchumi,kuwa washitakiwa wote
kwa pamoja wanashitakiwa mnamo
tarehe isiyojulikana agost
mwaka huu majira
ya usiku wa
manane huko katika
kijiji cha nyamiliro
na vijiji mbalimbali
katika kata ya
katunguru wilayani sengerema
mkoani mwanza kwa kudhamilia
na kinyume cha
sheria waliingilia na
kuhalibu transifoma nane
zenye thamani ya
shilingi milioni nne
laki tano thelathini
na tatu elfu
sitini na saba
nukuta tatu tano mali
ya serikali ya
jamuhuli ya muungano
wa Tanzania na
hivyo kuzuia upatikanaji
wa huduma za
msingi.
Hata hivyo
washitakiwa wote kwa
pamoja hawakutakiwa kijibu
chochote kwa kuwa
mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza
kesi ya uhujumu
uchumi mpaka ipate
izini ya
mkurugenzi wa makosa
ya jinai na
washitakiwa wote wamerudishwa
rumande hadi septemba
12 mwaka huu
kesi hiyo itatajwa
mahakamani hapo.
Na ,Joyce
Rollingstone,
Comments
Post a Comment