WANANCHI WANUFAIKA KUPITIA KILIMO CHA MUHOGO WILAYANI SENGEREMA.
Imeelezwa
kuwa wananchi wameonyesha mwamko wa
kulima zao la muhogo kutokana na zao hilo kuwa la kibiashara katika wilaya ya
Sengerema mkoa wa Mwanza.
Hayo
yamesemwa na wananchi wa kijiji cha Kijuka ambapo wameelezea zao la muhogo
limekuwa zao la biashara kutokana na
kupewa elimu na maafisa kilimo ngazi ya kata na wilaya hali iliyowalazimu kujikita
katika kulima zao hilo la muhogo.
Clip
wananchi…………..
Kwa
upande wake Afisa kilimo wilaya ya Sengerema SAIMON BUTELA amesema zao la muhogo ni kati ya mazao ambayo
yanastahimili ukame hivyo wakulima wanashauriwa kulima zao hilo ili wajiinue
kiuchumi.
Clip
afisa kilimo 1…………….
Pia
zao la muhogo ni zao la chakula na biashara hivyo wamekuwa wakitoa elimu kwa
wakulima ili waendelee kulima kilimo
hicho.
Clip
afisa kilimo 2……….
Aidha Bwn, Butera amewaomba maafisa ugani wa
kila kata kujipanga kuanza kutoa elimu kwa wakulima wao ili waweze kunufaika
kilimo na kuanza maandalizi ya kilimo mapema.
Na Deborah Maisa
Comments
Post a Comment