MWILI WA ASKARI
POLISI WAKUTWA UKIELEA NDANI YA ZIWA VICTORIA MANISPAA YA BUKOBA
Askari
polisi wa kitengo cha Intelijensia katika mkoa wa Kagera aliyefahamika kwa jina
la Mussa Salum Musanya amekutwa amefariki baada ya mwili wake kuokotwa ukielea
kwenye ufukwe wa ziwa Victoria katika eneo la Kiroyera manispaa ya Bukoba.
Askari
huyo wa polisi ambaye ameopelewa kwenye maji huku mwili wake ukiwa na sare za
jeshi la polisi alitoweka nyumbani kwake na kupotea katika mazingira ya
kutatanisha siku tatu zilizopita na kila walipomtafuta hakuweza kupatikana
mpaka mwili wake ulipokutwa ukielea kwenye fukwe ya ziwa Victoria.
Na Veronica Martine
pamoja sana
ReplyDelete