WATAKAOKAIDI KUJENGA CHOO
KUBURUZWA MAHAKAMANI WILAYANI SENGEREMA
Kamati ya mazingira ya
Kata Ibisabageni Wilayani Sengerema
imetangaza vita kali
kwa wananchi wanaokaidi
kujenga vyoo katika makazi yao
kwa kuwa hali hiyo inaweza
kusababisha magonjwa ya milipuko katika
siku za usoni .
Kauli hiyo imetolewa mjumbe wa
kamati ya mazingira ya kata
hiyo Bi,Martha Buta na mhasibu wa kamati hiyo
Bi . Emeryciana Patrick ambapo wamesema kuwa
baadhi ya wananchi hawajajenga
vyoo katika makazi yao wakisubili
kusukwa na serikali ili hali ni wajibu
wao kufanya hivyo.
Nae katibu wa mazingira
wa kata ya Ibisabageni Bwn,Paschael Ng’ombeyapi
amesema kuwa kwa
wale wanaokaidi kujenga vyoo
katika makazi yao watachukuliwa hatua kali za kisheria huku akiwaomba
wananchi kushirikiana kutunza mazingira .
Kuhusuana na suala la
upandaji miti Bwn, Ng’ombeyapi amewataka wananchi kupanda miti katika meneo yao ili kutunza mazingira
pindi msimu wa mvua utakapoanza .
Licha ya Baba wa Taifa
hayati Mwl,Julius Kambarage Nyelele kuanzisha kampeni ya panda mti kata
mti yenye lengo la kuhifadhi
mazingira zaidi ya miaka 15
iliyopita lakini imetajwa kampeni hiyo kusalia historia ya vitabuni pekee bila vitendo
katika baadhi ya maeneo hapa nchini.
Na Emmanuel Twimanye.
Comments
Post a Comment