KAMATA KAMATA YA BODABODA YAZUA TAHARUKI WILAYANI
SENGEREMA
Waendesha
pikipiki maarufu kama bodaboda wilayani Sengerema mkoani Mwanza wamelitupia
lawama jeshi la polisi kitengo cha
usalama barabarani wilayani Sengerema kwa
kile kinachodaiwa linashirikiana na kamanda wa waeendesha pikipiki kuwakamata bila
kufuata utaratibu na pikipiki zao kupelekwa sehemu isiyo rasimi hali iliyozua sintofahamu
kwa madereva hao.
Waendesha
bodaboda hao wamedai kuwa kumekuwa wakikamatwa bila kufuata utaratibu uliowekwa
hali iliyowalazimu kuitisha mkutano na viongozi wa umoja waendesha pikipiki
ngazi ya mkoa kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa kero hiyo.
Kufuatia
sakata hilo Radio sengerema imemtamtafuta Mratibu wa Elimu kwa umma kitengo cha
usalama barabarani Wilaya ya Sengerema Coplo Echika Mbozi ili kutolea
ufafanuzi suala hilo la kukamatwa waeendesha pikipiki ambapo amekana
madai hayo na kusema kuwa wanaolalamika ni watu ambao hawazingatii
sheria za usalama barabarani.
Malalamiko
ya kukamatwa waendesha pikipiki wilayani Sengerema yamekuwa ya muda mrefu hatimaye
yamepatiwa na idara husika.
Na Deborah Maisa
Comments
Post a Comment