KUNI ZA SABABISHA WANANCHI KULALAMIKA
Wananchi wa kijiji cha Ikoni kata ya Buzilasoga Wilayani Sengerema ,wamemtupia lawama mwalimu mkuu wa shule ya
msingi Ikoni Evaline Mkando kwa kuwaagiza
wanafunzi kuni pamoja na maji hali
ambayo imeleta sintofahamu kwa wazazi.
Wananchi
hao wametoa malalamiko hayo kwa mbunge wa jimbo la Sengerema Mh,William Mganga Ngeleja alipotembelea kijiji hicho ambapo wamedai mwalimu
huyo amekuwa akiwaagiza watoto kuni pamoja na maji hali iliyowalazimu wazazi kuhoji
kuni hizo zinafanya kazi gani shuleni hapo.
Akijibu
malalamiko hayo ya wananchi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikoni EVALINE
MKANDO amesema katika shule yao
kuna utaratibu ambao wanaufanya
wa kuwaagiza wanafunzi kuni kwa ajili ya
kupikia chakula wakati
wa mitihani.
Aidha Mwalimu mkuu huyo amesema maji hayo hutumika kuwasaidia wanafunzi kufanya usafi wa madarasa
kwa kuwa madarasa
hayana sakafu.
Na Deborah Maisa.
Comments
Post a Comment