WAKAZI WA KATA YA IBONDO WILAYANI SENGEREMA WAJITOLEA KUCHIMBA MTARO WA MAJI
Diwani wa kata ya Ibondo
Wilayani
Sengerema Mathias Mashauri kwa kushirikiana na wananchi wa kata yake wameamua
kuchimba bomba la maji ili kupata huduma ya maji katika kata hiyo kutokana na adha ya uhaba wa maji inayowakabili kwa muda mrefu.
Hayo yamebainika
wakati jitihada hizo za kuchimba bomba
la maji zikiendelea, diwani huyo amesema
kuwa lengo la kuwahamasisha wananchi
wake ni kuondoa changamoto
ya maji iliyokuwa inawakabili wananchi
hao kwa muda mrefu.
Hata hivyo Mh,Diwani ameipongeza serikali kwa
kuleta maji ya bomba katika kata
hiyo hali iliyowasaidia wananchi
Nao wananchi wa
kijiji hicho wameelezea namna
hali ya maji inavyowasibu katika
kijiji hicho.
Comments
Post a Comment