MAMA ALALA NJE BAADA YA KUUZWA KINYEMELA KIWANJA CHA MAKAZI .
Mama mwenye
watoto tisa amelazimika kulala
nje kwa
muda mrefu , baada ya baba wa familia kumtumia
rafiki yake kuuza kiwanja cha
familia yake kinyemela na kutokomea kusikojulikana wakati
mama wa familia na watoto wakiwa shambani
kwa shughuli za kilimo katika kitongoji cha Iseni kata ya Nyamizeze
Wilayani Sengerema.
Radio Sengerema imefika
katika eneo la familia hiyo ya Bwn Jumanne Sabuni
linalodaiwa kuuzwa na kuzungumza
na mama wa familia hiyo Bi, Lucia Kazila ambapo ameeleza kuwa akiwa shambani alikuta kiwanja hicho kimeuzwa
bila kupewa taarifa na mme
wake na kuanza kulala nje mpaka sasa.
Philipo
Mathias ni mwenyekiti wa
Kitongoji cha Iseni amekiri kuuzwa kwa eneo hilo kinyemela huku
akidai kuwa kwa sasa
anaendelea kufanyajitihada ili mama huyo apate hifadhi .
Nae afisa mtendaji wa kata ya Nyamizeze Bi. Mariam Simon akikiri
kupokea taarifa za
kuuzwa kwa kiwanja hicho
na kusema kuwa
atalipatia ufumbuzi suala hilo haraka iwezekanavyo ili mama huyo apate
makazi ya kudumu.
Comments
Post a Comment