DIWANI
ASHAMBULIWA KWA KUKATWA KATWA NA MAPANGA WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA
Diwani wa
Kata ya Nyakahanga wilayani Ngara mkoani Kagera, Charles Bechumila
ameshambuliwa kwa kuchomwa mishale ikiwa ni pamoja na kukatwa na panga na watu
wasiofahamika alipokuwa kwenye ziara.
Kiongozi
huyo anadaiwa alishambuliwa na watu wasiojulikana mapema leo alipokuwa kwenye
msafara wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mhe. Godfrey Mheluka uliokuwa
katika operesheni ya kuwaondoa watu wanaodaiwa kuvamia maeneo ya wafugaji
katika Kijiji cha Kashanda.
Katika
shambulizi hilo lililotokea leo Agosti 29 asubuhi, diwani wa Nyakahanga,
Charles Bechumila amejeruhiwa na amepelekwa katika Hospitali Teule ya
Nyakahanga.
Afisa
Tarafa ya Bugene Nyaishozi, Rozaria
Christian amesema walikuwa kwenye operesheni halali na wakulima hawakuwa
na taarifa hivyo baada ya kuwakamata wawili ndipo kundi la watu
lilijitokeza likionyesha kuwa lilijiandaa kuwashambulia.
Aidha
Christian amefafanua kwamba watu kadhaa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika
kumjeruhi diwani huyo na Mkuu wa wilaya hiyo, Mheluka amesema bado hayupo sawa
kuzungumzia tukio hilo.
Na Veronica Martine
Comments
Post a Comment