Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI aeleza walivyochunguza moyo wa Manji
Daktari katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu namna
walivyouchunguza moyo wa mfanyabiashara Yusuf Manji.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa
Mohammed Janabi (51) ametoa ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi ya
kutumia dawa za kulevya inayomkabili Manji.
Profesa Janabi ameieleza Mahakama
jinsi walivyoangalia vyuma vilivyopo kwenye moyo wa Manji kama vimeziba au la.
Akiwa shahidi wa kwanza wa upande wa
utetezi, Profesa Janabi aliongozwa na wakili Hajra Mungula kutoa ushahidi mbele
ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.
Manji ambaye katika hati ya mashtaka
jina lake ni Yusufali Manji, alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza
Februari 16 akidaiwa kati ya Februari 6 na 9 katika eneo la Sea View, Upanga
wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
Comments
Post a Comment