WILAYA
YA SENGEREMA YAKABILIWA NA UKOSEFU WA SHULE
Afisa tawala wa wilaya
ya sengerema bwana ,ARONI LAIZER amewapongeza wananchi wa kijiji cha ILEKANILO kata ya KASUNGAMILE kwa juhudi za kujitolea kujenga
shule ya msingi ya Bulyangele katika kijiji hicho.
Pongezi hizo
amezitoa wakati wa harambee ya kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ambaye
pia, alikuwa mgeni rasimi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Emmanuel Kipole na kusema kuwa wananchi wa kijiji hicho
wameonesha nia njema kwani hana budi
kuwashukuru.
Pia mgeni rasimi huyo
ameunga mkono juhudi za wananchi hao kwa
kutoa mifuko ishirini na moja ya
saruji itakayowasaidia kukamilisha
ujenzi wa shule ya Msingi Bulyangele.
Nae Mbunge wa
Jimbo la Sengerema Mh WILLIAM MGANGA NGELEJA
amewaunga mkono wananchi hao kwa kutuma mwakilishi wake na kuchangia mabati
mia moja ili kuezeka majengo yaliyobaki katika shule hiyo.
Sanjari na hayo Jumla
ya shilingi milioni tano na elfu arobaini na mifuko ishirini na nane zimepatikana katika harambe hiyo.
Na Charles Sungura
Comments
Post a Comment