DC AWANYOOSHEA KIDOLE WAKURUGENZI WATAKAOSHINDWA KUSIMAMIA MAENDELEO YA WANAFUNZI
Mkuu wa wilaya ya
Sengerema mkoani Mwanza Mh,Emmanuel Kipole
amewataka wakurugezi watendaji wa halimashauri ya
Sengerema na Buchosa pamoja
na maafisa elimu kutoa taarifa ya maendeleo ya wanafunzi.
Hayo ameyasema katika
baraza la madiwani wa halmashauri ya Buchosa ambapo mbunge wa jimbo la Buchosa
ambaye pia ni waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mh, Dkt.Charles Tizeba alipotaka kujua kama suala la utoro linafahamika kwenye Ofisi ya
mkurugenzi kwani katika shule ya Sekondari Lugata utoro umekithiri.
Hata hivyo mkuu wa
wilaya ya Sengerema Mh, Kipole amesema kumekuwepo na changamoto hiyo
ya utoro na wataalamu wa idara hiyo hawatoi taarifa ya maendeleo katika idara
zao.
Aidha Mkuu
wa wilaya amewata wazazi kushirikiana na walimu
katika kuhakikisha maendeleo ya
wanafunzi,huku akitoa taarifa kuhusu
kupanuliwa kwa shule ya sekondari nyehunge na kwamba mwaka huu itapokea wanafunzi wa kidato cha
tano kwa michepuo ya sanaa na sayansi .
Na Elisha Magege.
Na Elisha Magege.
Comments
Post a Comment