NYAVU HARAMU ZAWAPONZA WATU SITA WILAYANI SENGEREMA
Watu
sita wamefikishwa katika
mahakama ya wilaya
ya sengerema mkoani
mwanza kwa tuhuma
ya makosa mawili ya
kupatikana na nyavu
haramu.
Akisoma
shitaka linalowakabili mbele
ya hakimu wa
mahakama hiyo BI Monica
Ndyekobora .mwendesha
mashitaka wa jeshi
la polisi Inspecta
Slivesta Mwaiseje,amewataja washitakiwa
kuwa ni Kampichi Salvatory
mwenye umri wa
miaka 29 mkazi wa
nyakaliro, Simeo Raphael
mwenye umri wa
miaka 38 mkazi wa
Nyakaliro,Salvatory Mkwesa mwenye
umri wa miaka 60
mkazi wa Isenyi,Venancy
Masana mwenye umri
wa miaka 28 mkazi
wa Isenyi, na Fransisco Nicas mwenye umri
wa miaka 30 mkazi wa Lumeya.
Inspecta Mwaiseje ,amesema
kuwa kosa la kwanza washitakiwa
wote kwa pamoja
wanashitakiwa kwa kosa
la kupatikana na
nyavu haramu kinyume na
kifungu namba 66
kifungu kidogo cha 1
(A) na kifungu kidogo
cha 4 cha kanuni
za uvuvi ya
mwaka 2009 kinachotokana na kifungu
namba 57 cha sheria
ya uvuvi namba
22 ya mwka 2003 kuwa washitakiwa wote
kwa pamoja wanashitakiwa mnamo
agost 27 mwaka
huu majira ya
saa 4:00 huko katika
kijiji cha lugasa
wilayani sengerema mkoani
mwanza walipatikana na
nyavu haramu aina
ya timba
Kosa la pili washitakiwa wote
kwa pamoja wanashitakiwa kwa
kosa la kupatikana
na nyavu haramu kinyume na
kifungu namba 66
kifungu kidogo cha 1
(A) na kifungu kidogo
cha 4 cha kanuni
za uvuvi ya
mwaka 2009 kinachotokana na kifungu
namba 57 cha sheria
ya uvuvi namba
22 ya mwka 2003 kuwa washitakiwa wote
kwa pamoja wanashitakiwa muda ,tarehe na
eneo tajwa walipatikana
na nyavu haramu
aina ya kokolo.
Hata hivyo
washitakiwa wote kwa
pamoja wamekana kutenda
makosa hayo na
washitakiwa wote wamerudishwa
rumande kwa kushindwa
kutimiza masharta ya
mahakama na kesi hiyo
itatajwa septemba 12
mwaka huu kwa
maelezo ya awali
mahakmani hapo.
Na,Joyce Rollingstone
Comments
Post a Comment