WASIO KUWA NA VYOO VYA KUDUMU KUKIONA CHA MOTO -NYAMIZEZE -SENGEREMA. Afisa mtendaji wa Kata ya Nyamizeze Wilayani Sengerema Bi. Mnyang’ari Simon ametangaza msako mkali kwa wakazi wa kata hiyo ambao hawajajenga vyoo vya kudumu kwenye makazi yao ili kuepuka kukumbwa na magonjwa ya mlipuko. Bi,Mnyang’ari amefikia maamuzi ya kutangaza msako huo kutokana na uwepo wa mwamako hafifu wa kujenga vyoo huku, idadi kubwa ya wananchi wakijikita kujenga vyoo vya muda vilivyoezekwa kwa kutumia mabua ya mahindi. Kiongozi huyo ameweka wazi kuwa kwa yeyote atakaekamatwa hajajenga choo kwenye familia yake hatua kali za kisheria zitachukulia dhidi yake pasipo kujali ugumu wa maisha alionao kwani huduma hiyo ni kwa manufaa ya jamii. Hata hivyo katika hali ya kushangaza katika baadhi ya vitongoji vya kata ikiwemo Mwang’haranga baadhi ya familia hutegemea vyoo vya majirani na wanapokuta majirani hawapo kw
Posts
Showing posts from February, 2018
- Get link
- X
- Other Apps
DK.TIZEBA AWANYOOSHEA KIDOLE WAHUDUMU WA AFYA WILAYANI SENGEREMA. Wananchi wa vijiji vya Kasheka na Chamanyete vilivyoko katika kata ya Bangwe Halmashauri ya Buchosa wamekilalamikia kituo cha Afya cha Mwangika kwa utoaji mbovu wa huduma za afya. Hayo yamezungumzwa na wananchi katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Buchosa Dr,Charles John Tizeba ambaye pia ni Waziri wa Kilimo. Wananchi hao wamewatuhumu Mganga na wauguzi wa Kituo hicho kuwa na kauli mbaya kwa wagonjwa, pamoja na kutoa lisiti za kuandikwa kwa mkono kwa gharama za matibabu badala ya zile zinazo tolewa kwa mashine za kielektronik (EFD) . Malalamiko ya wananchi hao yakamlazimu Mbunge huyo kuwahakikishia wananchi kufuatilia suala hilo ambalo limeonekana kuwa kero kubwa kwa wananchi wanao fika katika kituo hicho kutafuta huduma ya matibabu. Pamoja na hayo Dr, Tizeba amechangia vifaa vya ujenzi kwenye sekta ya Afya na Elimu katika vijiji vya Kasheka na Chamanyete ikiwa ni
MBUNGE WA JIMBO LA SENGEREMA AWALILIA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KATUNGURU BAADA YA BWENI LA WAVULANA KUTEKETEA KWA MOTO
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza Mh, William Mganga Ngeleja ametembelea katika shule ya Sekondari Katunguru Iliyopo Wilayani Sengerema na kutoa pole kwa walimu na wanafunzi kufuatia tukio la bweni la wavulana kuteketea kwa moto hivi karibuni . Mh,Ngeleja akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo amesema taarifa za kuteketea kwa moto bweni hilo alizipata akiwa kwenye vikao vya bunge mjini Dodoma na kuzipokea kwa mshituko mkubwa . Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Katunguru Mwl. Baraka Ezekiel Msimba amemshukuru Mh,Ngeleja kwa michango yake mbalimbali ambayo amekuwa akitoa shuleni hapo ikiwemo mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa bweni lililoteketea kwa moto februari 6 mwaka huu Katika hatua nyingine baadhi ya walimu wa shule hiyo wamepata fursa ya kutoa changamoto zao zinazowakabili mbele ya mbunge wao. Pamoja na hayo Mh,Ngeleja pia ameahidi kufanya ukarabati wa
WAFANYABIASHARA WACHARUKA MBELE YA MBUNGE WAO WA JIMBO LA SENGEREMA
- Get link
- X
- Other Apps
Wafanyabiashara wa soko kuu mjini Sengerema mkoani Mwanza wamelalamikia kubomolewa vibanda vyao katika eneo la soko hilo wakitaka warudishiwe gharama zao walizo lipia . maisha ya wafanyabiashara baada ya kubomolewa vibanda vyao Malalamiko hayo yamekuja kufuatia siku chache baada kubomolewa vibanda vyao, ambapo Bw, Paschal Watosha ni mmoja wa wafanyabiashara hao amehoji kwa niaba ya wafanyabiashara katika mkutano na mbunge wa jimbo la Sengerema Mh, William Mganga Ngeleja uliofanyika katika mtaa wa Migombani Je, halmashauri itaawarudishia pesa zao walizolipia maeneo waliyokuwa wametengewa na halmashauri ? Akijibu Malalamiko hayo makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Sengerema bw, Sylivanus Bulapilo amesema kuwa wanaanza kuchukua hatua za kisheria kwa watumishi wao waliowapotosha wanachi kujenga vibanda hivyo kisha kubomolewa . Na,Amina Hassan
WATAALAMU NI DAWA YA KUKUZA MITI WILAYANI SENGEREMA
- Get link
- X
- Other Apps
Wananchi wanaofanya shughuli za upandaji miti Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuwaona wataalamu wa misitu ili kuongeza ubora katika zao hilo. Akiongea na Radio Sengerema ofisini kwake Meneja Wakala misitu Wilayani Sengerema Bwn, Urio Jeremia amesema, kwa takwimu zilizopo wilaya ya Sengerema imekuwa na kasi kubwa ya upandaji miti,na hivyo wanapaswa kufika katika Ofisi za wataalam kwa ushauri zaidi. Aidha Bwn Urio amebainisha miti inapaswa kupunguziwa matawi ili kuipa nafasi ya kunenepa kwa lengo la kupata mazao ya miti yenye ubora. Na,Michael Mgozi
WAFANYA USAFI MJINI SENGEREMA WAANGUA KILIO MBELE YA MBUNGE WAO
- Get link
- X
- Other Apps
Wafanya usafi mjini Sengerema wameilalamikia halmashauri ya Sengerema kwa kutowalipa stahiki zao kwa zaidi ya miezi minne sasa hali iliyopelekea wakose mahitaji ya kujikimu. Wafanya usafi mjini sengerema wakitekeleza majukumu yao Hayo yameyabainisha na wafanyakazi hao katika mkutano wa hadhara wa wananchi mjini Sengerema na mbunge wa jimbo hilo Mh, William Mganga Ngeleja uliofanyika mtaa wa migombani kata ya Nyampulukano na kwamba licha ya kuendelea na kazi yao mpaka sasa hawajui ni lini watapata stahiki zao ili wapate mahitaji yao ya kila siku. Kilio hicho cha wafanyakazi kimepokelewa na Mbunge wa jimbo hilo Mh, Ngeleja na kumuagiza mwenyekiti wa hamashauri kusimamia malipo ya wafanya usafi kwa kuwa wao ndio wanaolengwa na ilani ya chama tawala. Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Sengerema bw.Silvanus Bulapilo amesema kuwa mara KWA Mara amekuwa akipokea malalamiko
NEEMA YA DAWA YA PAMBA YALETWA KWA WAKULIMA WA PAMBA WILAYANI SENGEREMA
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya wakulima wa zao la pamba Wilayani Sengerema kulalamikia uhaba wa dawa ya kunyunyuzia Pamba hatimaye dawa hizo zimeletwa na na kupelekwa katika vituo husika ili wapewe wakulima. Akizungumza na Radio Sengerema ofisini kwake mwenyekiti wa kitongoji cha isugang’holo Bwn, Marco Sumuni amekiri kupokea dawa ya pamba kiasi cha chupa mia moja kwa ajili ya Wakulima wa pamba katika kitongoji hicho na kuwasihii wakulima kufuata dawa katika ofisi hiyo. Kwa upande mwingine mwenyekiti huyo amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kitongoji hicho wakidai kuwa dawa inayotewa haifanyi kazi. Aidha mwenyekiti huyo amewasihii wananchi wa kitongoji hicho kutumia dawa hiyo mara kwa mara ili kunusru mazao yao kuendelea kushambuliwa na wadudu. Hivi karibuni Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Emmanuel Kipole ametangaza kuletwa kwa dawa ya kunyunyuzia pamba Wi
WAZIRI MKUU MH,KASSIM MAJALIWA AZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO WILAYANI SENGEREMA NA KUACHA MAAGIZO MAZITO KWA VIONGOZI
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh,Kassim Majaliwa amezindua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Buchosa na Sengerema na kutoa maagizo mazito kwa wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote mbili . Waziri mkuu Mh, Kassim Majaliwa Maagizo hayo mazito ya waziri mkuu kwa wakurugenzi hao wawili yamekuja baada ya madiwani kumwambia waziri majliwa kuwa katika halmashauri ya Buchosa bado kuna utata wa miradi mitatu ya maji iliyoanzishwa mwaka 2012 ambapo hadi sasa miradi hiyo haijakamilika . Kufuatia malalamiko hayo waziri Majaliwa amemuagiza mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongella kwa kushirikiana na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Mwanza Athon Diaro kuhakikisha wanakaa pamoja na madiwani na wakurugenzi wa halmashaurio zote mbili kabla ya februari 23 mwaka huu. Awali akiwa katika Halmashauri ya Buchosa amezindua Miradi ya
WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA
- Get link
- X
- Other Apps
Akinamama wajawazito wilayani Sengerema mkoani mwanza wameombwa kuanza mapema chanjo ya pepopunda ili kumkinga mtoto alieko tumboni na ugonjwa huo. Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa kitengo cha afya Mama,baba na mtoto katika Hospitali Teule ya wilaya ya Sengerema Bi, Aloycia Kyaluzi wakati akiongea na Radio Sengerema amesema akinamama wajawazito wanatakiwa kuhudhuria mapema kwenye vituo vya afya ili kupatiwa chanjo hiyo. Hata hivyo Kyaluzi amewasisitiza mabinti kuhudhuria kwenye kituo cha afya ili kupatiwa chanjo ya pepopunda. Sambamba na hayo mtaalamu huyo amewataka kumaliza dozi ya chanjo hiyo ili kumshambulia mdudu huyo. Na , BWIZA BONIPHACE
WAZIRI MKUU MH, KASSIM MAJALIWA ATARAJIWA KUTINGA WILAYANI SENGEREMA KESHO FEBRUARI 15 2018
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kesho februari 15 mwaka huu. Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh, Emmanuel Kipole kwa vyombo vya habari waziri Majaliwa atawasili majira ya saa tisa alasiri na kuzindua kiwanda kidogo cha kuongeza thamani mazao ya nafaka Eneo la Bukala . waziri mkuu kassim Majaliwa Hii ni mara ya kwanza kwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania Mh, Kassim Majaliwa kuzulu Wilayani Sengerema tangu alipoingia madarakani katika serikali ya awamu ya tano . Na, EMMANUEL TWIMANYE
WIZARA YA HABARI YAWAFUNDA WAANDISHI WA HABARI NCHINI
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amewataka waandishi wa habari nchini kuzingatia maadili kwa kuandika habari zenye ukweli na uhakika kwa manufaa ya Taifa na Watanzania kwa ujumla. Shonza ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya Redio Duniani, ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na waandishi na watangazaji wa redio za jamii kutoka mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro, Mtwara, Shinyanga, Songwe, Geita, Mwanza, Kagera, Dodoma, Pemba, Unguja, Lindi na Songwe. “Redio za jamii zimekuwa tegemeo kubwa la kupata habari kwa wananchi wa maeneo mbalimbali hapa nchini hasa pembezoni mwa nchi. Mwananchi haitaji kuwa na umeme anapotaka kusikiliza Redio,” alisema Shonza. Amesema, ni vyema waandishi wawe wa kweli wanapotoa habari mbalimbali kwa wananchi ili kuepuka machafuko ya nchi kama ilivyotokea nchini Rwanda, ambapo chanzo cha machafuko hayo kilitokana na habari zilizotangazwa kupitia Redio. “Wananchi wanategemea habari toka k
WATAKIWA KUJITOLEA NGUVU KAZI KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NYANG'HWALE GEITA
- Get link
- X
- Other Apps
Wananchi Wilayani Nyang’hwale mkoani Geita wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kujitolea nguvu zao katika ujenzi wa vituo vya afya na zahanati kwa kila kata ifikapo Desemba 2018 Akitoa maelekekezo hayo mbele ya madiwani mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Nyang’hwale Bw,Caros Gwamagobe amesema kumekuwa na vifo visivyokuwa vya lazima hasa kwa mama wajawazito na watoto kutokana na huduma kuwa mbali na wananchi hivyo kila kijiji kinatakiwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya pamoja na Zanati kwa kila kata. Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Bw,Hamim Gwiyama amesema kijiji au kata ambayo haitashiriki katika kujenga vituo vya afya viongozi wote wa eneo hilo watawajibishwa kisheria. Hata hivyo madiwani wameahidi kushirikiana na wananchi katika kukamilisha ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya . Na ANNA ELIAS
WATAKAO GOMEA NYUMBA ZAO KUPULIZIWA DAWA YA UKOKO KUKIONA CHA MOTO WILAYANI SENGEREMA
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Mh,Emmanuel Kipole ametangaza vita kali kwa wananchi watakaogomea zoezi la upuliziaji dawa ya ukoko majumbani mwao linalotarajiwa kuanza Februari 14 hadi Machi 13 mwaka huu. Mkuu wa Wilaya ametoa tamko hilo zito wakati akizindua rasimi zoezi hilo muhimu la upuliziaji wa dawa ya ukoko majumbani kwa Mkoa wa Mwanza mradi unaotekelezwa na Halmashauri tatu za mkoa huo ambazo ni halmashauri ya Sengerema , Buchosa na Kwimba ili kuangamiza mbu wanaoeneza vimelea vya maambukizi ya Malaria. Ametaja takwimu za Malaria za mwaka 2016 katika Mkoa wa Mwanza kwa halmashauri hizo tatu ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema imeonyesha kuwa na asilimia 10.1 ya maambukizi ya malaria , Halmashauri ya Buchosa ni asilimia 12.7 huku Halmashauri ya kwimba ikiwa na asilimia 11.