NEEMA YA DAWA YA PAMBA YALETWA KWA WAKULIMA WA PAMBA WILAYANI SENGEREMA
Baada ya
wakulima wa zao la pamba
Wilayani Sengerema kulalamikia uhaba wa
dawa ya kunyunyuzia Pamba hatimaye dawa hizo zimeletwa
na na kupelekwa
katika vituo husika ili wapewe wakulima.
Akizungumza na Radio Sengerema ofisini kwake mwenyekiti
wa kitongoji cha isugang’holo Bwn, Marco
Sumuni amekiri kupokea dawa ya pamba kiasi cha chupa mia moja kwa ajili
ya Wakulima wa pamba
katika kitongoji hicho na
kuwasihii wakulima kufuata dawa katika ofisi hiyo.
Kwa upande mwingine mwenyekiti huyo amekiri
kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi
wa kitongoji hicho wakidai kuwa
dawa inayotewa haifanyi kazi.
Aidha mwenyekiti huyo
amewasihii wananchi wa kitongoji hicho kutumia dawa hiyo mara kwa mara ili kunusru mazao yao kuendelea kushambuliwa na
wadudu.
Hivi karibuni Mkuu wa
wilaya ya Sengerema Mh,Emmanuel
Kipole ametangaza kuletwa kwa dawa ya kunyunyuzia pamba Wilayani Sengerema na kuwataka wakulima waitumie kwa matumizi
sahihi.
Kuletwa kwa dawa ya kunyunyuzia pamba wilayani
sengerema hali hiyo itachagiza wakulima kunufaika na zao la pamba hapo
baadae.
Na, Tumain John
Comments
Post a Comment