WAFANYA USAFI MJINI SENGEREMA WAANGUA KILIO MBELE YA MBUNGE WAO
Wafanya usafi
mjini Sengerema wameilalamikia
halmashauri ya Sengerema kwa kutowalipa stahiki zao kwa zaidi ya miezi minne sasa hali
iliyopelekea wakose mahitaji ya kujikimu.
Wafanya usafi mjini sengerema wakitekeleza majukumu yao |
Hayo yameyabainisha na wafanyakazi hao katika mkutano wa hadhara wa wananchi mjini Sengerema
na mbunge wa jimbo hilo Mh, William Mganga
Ngeleja uliofanyika mtaa wa migombani kata ya Nyampulukano na kwamba licha ya
kuendelea na kazi yao mpaka sasa hawajui ni lini watapata stahiki zao ili wapate mahitaji yao ya kila siku.
Kilio hicho cha
wafanyakazi kimepokelewa na Mbunge wa
jimbo hilo Mh, Ngeleja na kumuagiza
mwenyekiti wa hamashauri kusimamia
malipo ya wafanya usafi kwa kuwa wao
ndio wanaolengwa na ilani ya chama tawala.
Kwa upande wake Makamu
mwenyekiti wa halmashauri ya Sengerema bw.Silvanus Bulapilo amesema kuwa mara KWA Mara
amekuwa akipokea malalamiko ya madai kutoka kwa wafanya kazi hao na
kwamba atahakikisha fedha zao zinapatikana.
Na,Amina Hassan
Comments
Post a Comment