WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA
Akinamama wajawazito
wilayani Sengerema mkoani mwanza wameombwa kuanza mapema chanjo ya
pepopunda ili kumkinga mtoto alieko tumboni na ugonjwa
huo.
Hayo yamebainishwa na
mtaalamu wa kitengo cha afya Mama,baba na mtoto katika Hospitali Teule ya
wilaya ya Sengerema Bi, Aloycia Kyaluzi wakati akiongea na Radio Sengerema amesema
akinamama wajawazito wanatakiwa kuhudhuria mapema kwenye vituo vya afya ili kupatiwa chanjo hiyo.
Hata hivyo Kyaluzi amewasisitiza
mabinti
kuhudhuria
kwenye kituo cha afya ili kupatiwa
chanjo ya pepopunda.
Sambamba na hayo
mtaalamu huyo amewataka kumaliza dozi ya chanjo hiyo ili kumshambulia
mdudu huyo.
Na , BWIZA BONIPHACE
Comments
Post a Comment