WATAKAO GOMEA NYUMBA ZAO KUPULIZIWA DAWA YA UKOKO KUKIONA CHA MOTO WILAYANI SENGEREMA
Mkuu wa Wilaya ya
Sengerema Mkoani Mwanza Mh,Emmanuel
Kipole ametangaza vita
kali kwa wananchi
watakaogomea zoezi la
upuliziaji dawa ya
ukoko majumbani mwao
linalotarajiwa kuanza Februari 14 hadi Machi 13
mwaka huu.
Mkuu wa
Wilaya ametoa tamko
hilo zito wakati
akizindua rasimi zoezi hilo
muhimu la upuliziaji wa dawa ya ukoko majumbani kwa Mkoa wa
Mwanza mradi unaotekelezwa
na Halmashauri tatu za mkoa huo
ambazo ni halmashauri ya Sengerema ,
Buchosa na Kwimba ili
kuangamiza mbu wanaoeneza
vimelea vya maambukizi
ya Malaria.
Ametaja takwimu za
Malaria za mwaka 2016
katika Mkoa wa Mwanza kwa
halmashauri hizo tatu ambapo Halmashauri ya Wilaya
ya Sengerema imeonyesha kuwa na asilimia 10.1 ya maambukizi ya malaria , Halmashauri ya Buchosa ni asilimia
12.7 huku Halmashauri ya kwimba ikiwa na asilimia 11.4
Mh, Kipole
amesema kuwa kuna baadhi ya
wananchi wamekuwa na mitazamo
potofu kuwa dawa
hizo zinasababisha kuleta wadudu aina ya kunguni hivyo
ametupilia mbali madai hayo na
kusema kuwa maneno hayo hayana ukweli
ndani yake.
Katika hatua nyingine Mh,Kipole amewaagiza viongozi wote wa halmashauri hizo tatu kuhamasisha na kusimamia zoezi hilo kwa weledi pamoja
na kamati zote za Wilaya
za ulinzi na usalama kuanzia ngazi
za wilaya kuhakikisha hakuna upotevu wowote
wa mali za wananchi na
kulinda usalama wa viuatilifu
hivyo kwani dawa hizo ni kwa ajili ya kuangamiza mbu na si vinginevyo.
Mkuu wa wilaya
amewaomba wananchi kutoa ushirikiano mkubwa katika zoezi hilo muhimu huku akiishukuru wizara ya afya pamoja na
wahisani kutoka nchini Marekani USAID kwa kuwezesha zoezi hilo.
Zoezi la upuliziaji
dawa ya ukoko majumbani linatarajiwa kuzifikia Jumla ya kaya laki mbili ,ishirini na tatu elfu na mia tisa na
tano zilizopo katika
halmashauri tatu zinazotekeleza mradi
huo ambazo ni Sengerema , Buchosa na
Kwimba.
Uzinduzi wa Zoezi hilo
umefanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya
ya sengerema .
Na, Emmanuel Twimanye
Comments
Post a Comment