WAZIRI MKUU MH,KASSIM MAJALIWA AZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO WILAYANI SENGEREMA NA KUACHA MAAGIZO MAZITO KWA VIONGOZI
Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mh,Kassim Majaliwa
amezindua miradi mbalimbali ya
Maendeleo katika Halmashauri ya Buchosa
na Sengerema na kutoa maagizo
mazito kwa wakurugenzi watendaji wa
halmashauri zote mbili .
Waziri mkuu Mh, Kassim Majaliwa |
Maagizo hayo
mazito ya waziri mkuu kwa wakurugenzi hao wawili
yamekuja baada ya madiwani
kumwambia waziri majliwa kuwa
katika halmashauri ya Buchosa bado kuna utata wa miradi
mitatu ya maji iliyoanzishwa mwaka 2012 ambapo hadi sasa miradi hiyo haijakamilika .
Kufuatia malalamiko hayo waziri Majaliwa
amemuagiza mkuu wa mkoa wa mwanza
John Mongella
kwa kushirikiana na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Mwanza
Athon Diaro kuhakikisha
wanakaa pamoja na madiwani na wakurugenzi wa halmashaurio zote mbili
kabla ya februari 23 mwaka huu.
Awali
akiwa katika Halmashauri ya Buchosa
amezindua Miradi ya
jengo la Hospitali ya Halmashauri
ya Buchosa , lenye zaidi
ya thamani ya shilingi
Milioni 300 na
Mabweni ya wasichana ya Nyehunge
Sekondari kwa kidato cha tano na
sita huku katika halmashauri ya Sengerema
akindua kiwanda kidogo cha
kuongeza thamani mazao ya Nafaka
kilichopo eneo la Bukala Mjini Sengerema
Comments
Post a Comment