WASIO KUWA NA VYOO VYA KUDUMU KUKIONA CHA MOTO -NYAMIZEZE -SENGEREMA.

Afisa   mtendaji   wa   Kata  ya   Nyamizeze     Wilayani  Sengerema    Bi.  Mnyang’ari    Simon  ametangaza  msako  mkali  kwa  wakazi  wa kata hiyo  ambao  hawajajenga  vyoo  vya kudumu  kwenye makazi yao ili kuepuka kukumbwa  na   magonjwa ya mlipuko.  
Image result for picha za ujenzi wa vyoo
 
Bi,Mnyang’ari  amefikia maamuzi  ya kutangaza msako huo kutokana na uwepo wa mwamako hafifu  wa kujenga vyoo huku, idadi kubwa  ya     wananchi    wakijikita   kujenga    vyoo vya muda  vilivyoezekwa   kwa  kutumia   mabua ya mahindi.

Kiongozi huyo  ameweka wazi kuwa   kwa yeyote atakaekamatwa   hajajenga   choo kwenye familia yake   hatua kali za kisheria  zitachukulia  dhidi yake  pasipo kujali ugumu wa maisha alionao kwani  huduma hiyo  ni   kwa manufaa  ya jamii.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza katika baadhi ya vitongoji  vya kata  ikiwemo Mwang’haranga  baadhi ya familia  hutegemea vyoo vya majirani  na wanapokuta majirani hawapo kwenye familia zao hulazimika  kwenda kujihifadhi porini.

Na, Emmanuel                                           

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA