DK.TIZEBA AWANYOOSHEA KIDOLE WAHUDUMU WA AFYA WILAYANI SENGEREMA.
Wananchi wa vijiji vya
Kasheka na Chamanyete vilivyoko katika
kata ya Bangwe Halmashauri ya Buchosa
wamekilalamikia kituo cha Afya cha Mwangika kwa utoaji mbovu wa huduma za afya.
Hayo yamezungumzwa na
wananchi katika mkutano wa hadhara wa
mbunge wa jimbo la Buchosa Dr,Charles John Tizeba ambaye pia ni Waziri wa
Kilimo.
Wananchi hao wamewatuhumu
Mganga na wauguzi wa Kituo hicho kuwa na kauli mbaya kwa wagonjwa, pamoja na kutoa lisiti za kuandikwa kwa mkono
kwa gharama za matibabu badala ya zile zinazo tolewa kwa mashine za kielektronik (EFD) .
Malalamiko ya wananchi
hao yakamlazimu Mbunge huyo kuwahakikishia wananchi kufuatilia suala hilo ambalo
limeonekana kuwa kero kubwa kwa wananchi wanao fika katika kituo hicho kutafuta
huduma ya matibabu.
Pamoja na hayo Dr, Tizeba amechangia vifaa vya
ujenzi kwenye sekta ya Afya na Elimu katika vijiji vya Kasheka na
Chamanyete ikiwa ni sehemu ya kuunga
mkono shughuli za maendeleo katika jimbo hilo.
Waziri Tizeba
anaendelea na Ziara ya kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumchagua kuwa
mbunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,sambamba na kutatua changamoto zinazo
wakabili wananchi .
Na; KATEMI
Comments
Post a Comment