MBUNGE WA JIMBO LA SENGEREMA AWALILIA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KATUNGURU BAADA YA BWENI LA WAVULANA KUTEKETEA KWA MOTO
Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza Mh, William Mganga Ngeleja ametembelea katika shule ya Sekondari Katunguru Iliyopo Wilayani Sengerema na kutoa pole kwa walimu na wanafunzi kufuatia tukio la bweni la wavulana kuteketea kwa moto hivi karibuni .
Mh,Ngeleja
akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo amesema taarifa za kuteketea kwa moto bweni
hilo alizipata akiwa
kwenye vikao vya bunge mjini Dodoma na kuzipokea kwa mshituko mkubwa .
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Katunguru Mwl. Baraka Ezekiel Msimba amemshukuru Mh,Ngeleja kwa michango yake mbalimbali ambayo amekuwa akitoa shuleni hapo ikiwemo mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa bweni lililoteketea kwa moto februari 6 mwaka huu
Katika hatua nyingine baadhi ya walimu wa shule hiyo wamepata fursa ya kutoa changamoto zao zinazowakabili mbele ya mbunge wao.
Pamoja na hayo Mh,Ngeleja pia ameahidi kufanya ukarabati wa barabara inayoelekea shuleni hapo ili kuondoa adha ya ubovu wa barabara inayowakumba wanafunzi wa shule hiyo .
Na,Thobis Ngubila
Na,Thobis Ngubila
Comments
Post a Comment