WATAKIWA KUJITOLEA NGUVU KAZI KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NYANG'HWALE GEITA
Wananchi Wilayani
Nyang’hwale mkoani Geita wametakiwa kushiriki
kikamilifu katika kujitolea nguvu zao katika ujenzi wa vituo vya afya na
zahanati kwa kila kata ifikapo Desemba 2018
Akitoa maelekekezo hayo
mbele ya madiwani mkurugenzi mtendaji wa
wilaya ya Nyang’hwale Bw,Caros Gwamagobe amesema kumekuwa na vifo visivyokuwa
vya lazima hasa kwa mama wajawazito na watoto
kutokana na huduma kuwa mbali na wananchi hivyo kila kijiji kinatakiwa
kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya pamoja na Zanati kwa kila kata.
Kwa upande wake mkuu wa
wilaya ya Nyang’hwale Bw,Hamim Gwiyama amesema kijiji au kata ambayo
haitashiriki katika kujenga vituo vya afya viongozi wote wa eneo hilo
watawajibishwa kisheria.
Hata hivyo madiwani
wameahidi kushirikiana na wananchi katika kukamilisha ujenzi wa vituo vya
kutolea huduma za afya .
Na ANNA ELIAS
Comments
Post a Comment