Posts

ADHA YA MAJI YA ENDELEA KUWATESA WANANCHI WILAYANI SENGEREMA

Image
Wananchi wa kijiji cha tunyenye kata ya kishinda wilayani sengerema mkoani mwanza  wamelalamikia ukosefu wa maji katika kijijini hicho. Wananchi wa Kijiji hicho wakizungumza na Radio Sengerema kwa nyakati tofauti  wamesema kuwa wanalazimika kufuata maji umbali mrefu hali ambayo imekuwa ikiwalazimu  kuamka usiku wa manane kufuata huduma hiyo katika vijiji vya jirani kwa upande wake ,mwenyekiti wa kijiji hicho Bwn,William   Mussa Makeja amekili kukosekana kwa  maji katika kijiji hicho  ambapo amesema   kunakisima kimoja lakini hata hivyo  akikidhi mahitaji ya wananchi wake. Adha ya maji inadaiwa kuwa bado ni  tatizo kubwa kwa wakazi wilayani Sengerema hususani wanao ishi vijijini licha ya wilaya hiyo kuwa na neema ya kuzungukwa na maji ya  Ziwa victoria  Na Neema Sammuson                 

Kamati ya siasa mkoa wa mwanza ya kagua miradi ya maendeleo wilaya ya Sengerema

Image
Mwenyekitiwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani mwanza Bwn,Antony Diallo amewataka wakurugenzi wahalmashauri wilayani sengerema mkoani Mwanza kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya maji na yote kutekelezwa na serikali kwa ajili ya wananchi. Dkt Diallo amesema kuwa katika kuhakikisha miradi inakamilika na kuwanufaisha wananchi kama sehemu yautekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi wataalamu wahalmashauri zote za Sengerema na Buchosa wanapaswa kushirikiana na wakandarasi kwakusharauriana nakutumia vifaa imara ili miundombinu itumike kwa muda mrefu baada ya kukamilika. Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kata ya Buyagu wakizungumza mara baada ya ziara ya kiongozi kutembelea mradi wa maji wa kalangala na Bitoto wamesema kuwa serikali inapaswa kufanya ufuatiliaji wakaribu ilikukamilisha mradi huo na kwamba kwa sasa wanatumia maji ya ziwa ambayo si salama hali inayo waongezea hofu nakujiona kama wanasahaulika. Mhandisi wa maji halmashauri ya Sengerema amesema kuwa w

ADHA YA MAJI YAWATESA WAKAZI WA SENGEREMA TANGU MWAKA 1974

Image
Akinamama  katika kijiji cha Kasomeko  Wilayani Sengerema  wanalazimika kuamka usiku wa manane kwenda kusaka maji  katika ziwa victoria   kutokana na kukabiliwa na tatizo la uhaba wa huduma hiyo tangu mwaka 1974. Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wameieleza Radio   Sengerema kuwa   wanashangazwa  na kitendo cha kukumbwa na kadhia ya maji   kwa muda mrefu  licha ya  kuishi   karibu  na mwambao  wa ziwa Victoria,  huku wakiwatupia lawama viongozi wa kisiasa  waliowachagua kwa kuwapa ahadi  ya kuwaletea maji   bila mafanikio . Kwa upande wake  mwenyekiti wa kijiji hicho Bw,Masanyiwa Charles  amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la maji katika kijiji chake na  kusema kuwa   licha ya kuahidiwa  na viongozi hao wa kisiasa kuwa watawaletea neema ya maji lakini hadi sasa ukimya bado umetanda na kulazimika kmpigia simu Diwani wa kata ya katunguru Methew Lubongeja mbele ya waandishi  ili kujua hatima ya maji katika  eneo lake . Aidha  huu ni wakati mzuri  kwa viongozi wa kisiasa  kut

WAWILI WAFARIKI KWA WIVU WA MAPENZI SENGEREMA

Image
WAWILI WAFARIKI KWA WIVU WA MAPENZI SENGEREMA Mwanaume mmoja amuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake kisha na yeye kujichoma kisu tumboni na kufariki dunia katika kijiji cha Kanyara Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza Wanandoa hao   waliopoteza maisha ni   Michael Daud mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa kijiji cha Bukokwa na Mkewe Teleza Kamli Mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa kijiji cha Bukokwa wilayani Sengerema. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji cha Msikitini katika kijiji cha Kanyara   Samora Mayila Makubi amesema Tukio hilo   limetokea Juni 19 mwaka huu saa 11 alfajiri katika Nyumba ya   kulala wageni ya New Enjoy   iliyopo kijiji cha kanyara ambapo wanandoa hao walenda kulala kwa ajili ya mapunziko. Amesema wanandoa hao wanandaiwa kuwa na mgogoro wa kifamilia kwa muda mrefu hali ambayo ilipelekea mwanamke kurudi kwao kijiji cha kanyara ambapo mumewe   alianz

WATUMISHI WA NNE WATUMBULIWA BUCHOSA

Image
Baraza la madiwani  katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoani Mwanza   limewafukuza kazi watumishi wanne kutokana na kuwa na  makosa ya utoro kazini pamoja na makosa ya jinai. Akitoa adhabu hiyoMwenyekiti wa halmashauri   Joseph   Kanyumi   kupitia baraza la madiwani kamati ya mamlaka ya nidhamu, kutokana na makosa hayo, kwa mjibu wa kanuni ya 42 (a)  kanuni ya utumishi wa Umma   ya mwaka 2003 aina ya makosa Adhabu zimeainishwa ikiwemo kufukuzwa kazi,kupunguziwa mshahara au kushushwa cheo. Aidha amewataja watumishi hao kuwa ni Thobias Kahindi ,Aloyce   Lukas Ngomeni,ambao walikuwa ni Maafisa watendaji wa vijiji wote wawili walipatikana na makosa ya   jinai, wengine ni Marko Mwanzalima Afisa Mtendaji wa kijiji,Godson Elisal yeye ni tabibu msaidizi ambao kwa pamoja walikutwa na kosa la utoro kazini. Katika hatua nyingine baraza hilo limetoa   onyo kwa Samweli Mgeta ambaye ni Afisa mtendaji wa kijiji,Kanyumi alipohojiwa kuhusu utambuzi wa vituo vyao vya
Watoto wawili wa familia moja katika kata ya Nyatukara wilayani Sengerema mkoani Mwanza wamefariki dunia  baada ya kuzama kwenye dimbwi lilopo katika mtaa wa Nyatukara. Walio patwa na mauti hayo wamejulikana kwa majina ya Taus John mwenye umri wa miaka kumi na tatu (13) na Tabu John miaka kumi na moja (11)  
Image
Wauguzi katika Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema   Mkoani Mwanza wameitaka Serikali kutatua changamoto zinazo wakabili katika maeneo yao ya kazi. Wamesema hayo wakati wakisoma risala katika kilele cha mazimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyo fanyika katika kituo cha Afya Nyehunge ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Froles Naiti Ngale mwanzilishi wa fani ya uuguzi takiribani   miaka 90 iliyo pita. Wamesema wamekuwa wakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa pamoja idadi ndogo ya wauguzi hali inayo pelekea kufanya majukumu amabayo siyo yao,kuhamishwa kwa watumishi bila kulipwa malipo yao  na kuondolewa kwenye vyama walivyo jiunga  na ku unganishwa kwenye vyama vingine pasipo lidhaa yao. Akijibu changamoto hizo Afisa Utumishi wa Halmshauri ya Buchosa Bi, Joyce Manyanda kwaniaba ya mkurungenzi wa halimashauri hiyo amesema Halmashuri ya Buchosa ina daiwa zaidi ya milioni miatatu (300,000,000) zinazo tokana na malimbikizo ya fedha za uhamisho wa watumishi walio hama kutok