ADHA YA MAJI YA ENDELEA KUWATESA WANANCHI WILAYANI SENGEREMA

Wananchi wa kijiji cha tunyenye kata ya kishinda wilayani sengerema mkoani mwanza  wamelalamikia ukosefu wa maji katika kijijini hicho.


Wananchi wa Kijiji hicho wakizungumza na Radio Sengerema kwa nyakati tofauti  wamesema kuwa wanalazimika kufuata maji umbali mrefu hali ambayo imekuwa ikiwalazimu  kuamka usiku wa manane kufuata huduma hiyo katika vijiji vya jirani

kwa upande wake ,mwenyekiti wa kijiji hicho Bwn,William Mussa Makeja amekili kukosekana kwa  maji katika kijiji hicho  ambapo amesema   kunakisima kimoja lakini hata hivyo  akikidhi mahitaji ya wananchi wake.

Adha ya maji inadaiwa kuwa bado ni  tatizo kubwa kwa wakazi wilayani Sengerema hususani wanao ishi vijijini licha ya wilaya hiyo kuwa na neema ya kuzungukwa na maji ya  Ziwa victoria 

Na Neema Sammuson                 



Comments

  1. Kwa nini shida ya maji inawasumbua wana sengerema wakati ziwa lipo kalibu kwa nini serikali isiwatengenezee visima

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA