Wauguzi katika Halmashauri ya Buchosa Wilayani
Sengerema Mkoani Mwanza wameitaka
Serikali kutatua changamoto zinazo wakabili katika maeneo yao ya kazi.
Wamesema hayo wakati wakisoma risala katika
kilele cha mazimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyo fanyika katika kituo cha
Afya Nyehunge ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Froles Naiti Ngale mwanzilishi wa
fani ya uuguzi takiribani miaka 90 iliyo
pita.
Wamesema wamekuwa wakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa
pamoja idadi ndogo ya wauguzi hali inayo pelekea kufanya majukumu amabayo siyo
yao,kuhamishwa kwa watumishi bila kulipwa malipo yao na kuondolewa kwenye vyama walivyo jiunga na kuunganishwa kwenye vyama vingine pasipo lidhaa yao.
Akijibu changamoto hizo Afisa Utumishi wa
Halmshauri ya Buchosa Bi, Joyce Manyanda kwaniaba ya mkurungenzi wa
halimashauri hiyo amesema Halmashuri ya Buchosa ina daiwa zaidi ya milioni miatatu (300,000,000) zinazo tokana na malimbikizo ya fedha za uhamisho wa watumishi walio hama kutoka Halmashauri ya Sengerema kwenda Halmashauri ya Buchosa
Hata hivyo ameongeza kuwa serikali imeanza kutatua baadhi ya changamoto kama vile upungufu wa watumishi ambapo serikali imetangaza hivi karibuni ajira katika Idara ya Afya, huku
changamoto nyingine akiahidi kuzichukua iliziweze kufanyiwa utatuzi wa haraka.
Mazimisho ya siku ya wauguzi duniani yamefanyika katika kata Nyehunge Halmashauri
ya Buchosa na kitaifa yamefanyika katika mkoa wa Mara huku kauli mbiu ikiwa ni ''Wauguzi
Sauti ya kuongoza,Afya ni haki ya Binadamu''
Na Katemi Renatus, Buchosa Sengerema
Na Katemi Renatus, Buchosa Sengerema
Comments
Post a Comment