WATUMISHI WA NNE WATUMBULIWA BUCHOSA
Baraza la madiwani
katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoani Mwanza limewafukuza kazi watumishi wanne kutokana
na kuwa na makosa ya utoro kazini pamoja
na makosa ya jinai.
Akitoa adhabu hiyoMwenyekiti wa halmashauri Joseph Kanyumi kupitia baraza la madiwani kamati ya mamlaka
ya nidhamu, kutokana na makosa hayo, kwa mjibu wa kanuni ya 42 (a) kanuni ya
utumishi wa Umma ya mwaka 2003 aina ya
makosa Adhabu zimeainishwa ikiwemo kufukuzwa kazi,kupunguziwa mshahara au kushushwa
cheo.
Aidha amewataja watumishi hao kuwa ni Thobias Kahindi
,Aloyce Lukas Ngomeni,ambao walikuwa ni
Maafisa watendaji wa vijiji wote wawili walipatikana na makosa ya jinai, wengine ni Marko Mwanzalima Afisa
Mtendaji wa kijiji,Godson Elisal yeye ni tabibu msaidizi ambao kwa pamoja
walikutwa na kosa la utoro kazini.
Katika hatua nyingine baraza hilo limetoa onyo kwa Samweli Mgeta ambaye ni Afisa
mtendaji wa kijiji,Kanyumi alipohojiwa kuhusu utambuzi wa vituo vyao vya kazi
hakuweza kufanya hivyo kutokana na ripoti aliyo ipokea kutoka Ofisi ya utumishi
haikuweza kubainisha vituo vyao vya kazi.
Na Katemi Renatus, Sengerema - Buchosa
Comments
Post a Comment