ADHA YA MAJI YAWATESA WAKAZI WA SENGEREMA TANGU MWAKA 1974
Akinamama katika kijiji cha Kasomeko Wilayani Sengerema wanalazimika kuamka usiku wa manane kwenda
kusaka maji katika ziwa victoria kutokana na kukabiliwa na tatizo la uhaba wa
huduma hiyo tangu mwaka 1974.
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wameieleza Radio Sengerema kuwa
wanashangazwa na kitendo cha
kukumbwa na kadhia ya maji kwa muda
mrefu licha ya kuishi
karibu na mwambao wa ziwa Victoria, huku wakiwatupia lawama viongozi wa kisiasa waliowachagua kwa kuwapa ahadi ya kuwaletea maji bila mafanikio .
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bw,Masanyiwa
Charles amekiri kuwepo kwa tatizo hilo
la maji katika kijiji chake na kusema
kuwa licha ya kuahidiwa na viongozi hao wa kisiasa kuwa watawaletea
neema ya maji lakini hadi sasa ukimya bado umetanda na kulazimika kmpigia simu
Diwani wa kata ya katunguru Methew
Lubongeja mbele ya waandishi ili
kujua hatima ya maji katika eneo lake .
Aidha huu ni wakati mzuri kwa viongozi wa kisiasa kutekeleza ahadi zao
walizowaahidi wananchi ili kutatua kero zinazowakabili wilayani Sengerema.
Na Emmanuel Twimanye
Na Emmanuel Twimanye
Comments
Post a Comment