WAWILI WAFARIKI KWA WIVU WA MAPENZI SENGEREMA
WAWILI WAFARIKI KWA WIVU WA MAPENZI SENGEREMA
Mwanaume mmoja amuua mkewe kwa kumchoma na kitu
chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake kisha na yeye kujichoma kisu
tumboni na kufariki dunia katika kijiji cha Kanyara Halmashauri ya Buchosa
Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza
Wanandoa hao
waliopoteza maisha ni Michael
Daud mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa kijiji cha Bukokwa na Mkewe Teleza Kamli
Mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa kijiji cha Bukokwa wilayani Sengerema.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti
wa kitongoji cha Msikitini katika kijiji cha Kanyara Samora Mayila Makubi amesema Tukio hilo limetokea Juni 19 mwaka huu saa 11 alfajiri
katika Nyumba ya kulala wageni ya New
Enjoy iliyopo kijiji cha kanyara ambapo
wanandoa hao walenda kulala kwa ajili ya mapunziko.
Amesema wanandoa hao wanandaiwa kuwa na mgogoro
wa kifamilia kwa muda mrefu hali ambayo ilipelekea mwanamke kurudi kwao kijiji
cha kanyara ambapo mumewe alianza kwenda
nyumbani kwao na mkewe mara kadha kwa ombi la kumtaka warudi nyumbani kwa ajili
ya kulea familia yao, ombi ambalo limekuwa litupiliwa mbali na mkewe.
Hata hivyo june 18 mwaka huu mumewe alirudi kwao
na mkewe kwa ombi hilo hilo na usiku ulipo ingia walienda kupumzika katika
nyumba ya kulala wageni ndipo alipo amua kufanya unyama huo.
Na, Katemi lenatus
Comments
Post a Comment