Kamati ya siasa mkoa wa mwanza ya kagua miradi ya maendeleo wilaya ya Sengerema
Mwenyekitiwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani mwanza Bwn,Antony Diallo amewataka wakurugenzi
wahalmashauri wilayani sengerema mkoani Mwanza kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi
ya maji na yote kutekelezwa na serikali kwa ajili ya wananchi.
Dkt Diallo amesema
kuwa katika kuhakikisha miradi inakamilika na kuwanufaisha wananchi kama sehemu
yautekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi wataalamu wahalmashauri zote za Sengerema
na Buchosa wanapaswa kushirikiana na wakandarasi kwakusharauriana nakutumia vifaa
imara ili miundombinu itumike kwa muda mrefu baada ya kukamilika.
Kwa upande wao
baadhi ya wananchi wa kata ya Buyagu wakizungumza mara baada ya ziara ya kiongozi
kutembelea mradi wa maji wa kalangala na Bitoto wamesema kuwa serikali inapaswa
kufanya ufuatiliaji wakaribu ilikukamilisha mradi huo na kwamba kwa sasa wanatumia
maji ya ziwa ambayo si salama hali inayo waongezea hofu nakujiona kama wanasahaulika.
Mhandisi wa maji
halmashauri ya Sengerema amesema kuwa wanaendelea kushirikiana kwa ukaribu na mkandarasi
natayari vifaa kwaajili ya ukamilishaji wamradi huo ndani ya muda mfupi mradi utaanza
kutoa huduma katika vijiji vya Buyangu,Kalangalala na Bitoto ambao umekamilika kwa
asilimia 70 na unatarajia kutoa huduma kwa wakazi wapatao 16,000 waliopo katika
vijiji hivyo, amesema umradi huo unatekelezwa na kampuni ya “D4N Co.Ltd”
utagharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 1,702,500,170
Awali wakiwa katika
Halmashauri ya Buchosa kamati hiyo imetembelea miradi ya maendeleo mbalimbali ukiwemo
ukarabatiwa kituo cha afya kome unaotekelezwa kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi
(RBF) ambao umegharimu shilingi milioni 400
Akiwa katika
Halmashauri ya Buchosa miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa maji wa
Lumeya,Kalebezo na Nyehunge ambapo Drt Anthony Diallo alitoa maelekezo kwa wasimamizi
wamiradi hiyo kuhakikisha inakamilika kwa wakati.
Comments
Post a Comment