WANAFUNZI WAGEUZA VICHAKA KUWA VYOO KATIKA HALMASHAURI YA BUCHOSA (W) SENGEREMA
Zaidi ya
wanafunzi 600 wa
shule ya msingi
ingwanzozu iliyopo katika
halmashauli ya buchosa
wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wanalazimiki kujihifadhi vichakani
kutokana na ukosefu
wa vyoo shuleni
hapo.
Wakizungumza
na passion fm wanafunzi wa Shule hiyo,wamesema wanakabiliwa na changamoto hiyo
baada ya vyoo vilivyo kuwepo kujaa hali ambayo imekuwa ikiwalazimu kwenda
kujihifadhi vichakani.
Wameongeza
kuwa kuwepo kwa hali hiyo shuleni hapo kuna weza kusababisha kutokea kwa
magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.
Michael
Danniel Onyanzo ni mwalimu mkuu wa shule hiyo,amekiri kuwepo kwa changamoto ya
ukosefu wa vyoo katika shule hiyo hali inayo pelekea wanafunzi kupata shida ya
kujihifadhi pindi wanapo hitaji huduma hiyo.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Bulashi amesema,kwa kukabiliana na changamoto hiyo
wamesha anza kujenga vyoo vingine kwa kutegemea nguvu kutoka kwa wawekezaji
waliopo kijijini hapo
Shule
ya Msingi Igwanzozu inakabiliwa na ukosefu wa vyoo kwa zaidi ya miaka
mitatu,huku jamii ikitajwa kugomea kuchangia ujenzi huo kwa madai ya kumtaka
aliye kuwa Afisa mtendaji wa kijiji hicho Charles
masele ambaye kwa sasa siyo mtendaji wa kijiji hicho arudishe fedha za
ujenzi wa choo zilizochangishwa na mtendaji huyo,ambapo kiasi cha fedha hakijawekwa wazi
Na Katemi Renatus; Buchosa Sengerema
Comments
Post a Comment