PESA YAWASABABISHA BODABODA KUTOA SADAKA MAISHA YAO WILAYANI SENGEREMA


Waendesha    Bodaboda  Wilayani  Sengerema  Mkoani Mwanza wametakiwa  kuacha   kujitoa  mhanga   kuhatarisha  maisha yao   kwa  kufanya kazi   nyakati  za  usiku. 


Image result for PICHA ZA WAENDESHA BODABODA
waendesha bodaboda  wakifanyakazi  nyakati za usiku   
Tahadhari hiyo  imetolewa  na jeshi la polisi   kitengo cha usalama barabarani Wilayani Sengerema  PC NORSHIRD  MUSSA  kufuatia   baadhi ya waendesha bodaboda kuendelea kukaidi agizo la serikali la kufanya kazi  mwisho saa    sita  usiku.

Kwa upande  wake   mwenyekiti wa  umoja wa waendesha   bodaboda wilaya ya Sengerema  Bwn,KANZU SELEMAN  na katibu wake    JOSEPHAT JOHN  wameunga mkono kauli  ya jeshi  la polisi  kwa kuwa kufanya hivyo  ni kinyume  cha sheria  za  nchi  pamoja na kuhatarisha   usalama wao.

Licha ya   serikali   kupiga marufuku    waendesha bodaboda    kufanya kazi   nyakati za usiku   ili kulinda  usalama wao   lakini suala hilo bado linaendelea wilayani  Sengerema.

Na,Emmanuel Twimanye  

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WAJAWAZITO WAPEWA MWAROBAINI WA KUMUOKOA MTOTO ALIEKO TUMBONI DHIDI YA UGONJWA WA PEPOPUNDA