UDONGO AINA YA PEMBA WATISHIA MAISHA YA MAMA NA MTOTO WILAYANI SENGEREMA.
Akina mama wametakiwa kuepuka utumiaji wa udongo aina ya Pemba pindi wanapokuwa na ujauzito kwani
husababisha madhara kwa mama na
mtoto, ikiwa ni pamoja na kujifungua mtoto kabla
ya wakati.
Rai hiyo
imetolewa na Kaimu Mganga Mfawidhi Kituo
cha Afya Sengerema Bi Regina Jackobo wakati akizungumza na Radio Sengerema
ofisini kwake.
Bi .Rejina ,amebainisha
kuwa ,utumiaji wa udogo aina ya pemba unasababisha mama mjamzito kupata
maambukizi ya minyoo hali ambayo hupelekea mtoto kuzaliwa akiwa na upungufu wa
damu, pamoja na uzito mdogo.
Hata hivyo,akina mama wajawazito wametakiwa
kuzingatia lishe bora na kuachana na matumizi ya pemba ili kulinda afya ya mtoto na mama kwa ujumla.
Na MICHAEL
MGOZI.
Comments
Post a Comment