WATUMISHI WA NNE WATUMBULIWA BUCHOSA
Baraza la madiwani katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoani Mwanza limewafukuza kazi watumishi wanne kutokana na kuwa na makosa ya utoro kazini pamoja na makosa ya jinai. Akitoa adhabu hiyoMwenyekiti wa halmashauri Joseph Kanyumi kupitia baraza la madiwani kamati ya mamlaka ya nidhamu, kutokana na makosa hayo, kwa mjibu wa kanuni ya 42 (a) kanuni ya utumishi wa Umma ya mwaka 2003 aina ya makosa Adhabu zimeainishwa ikiwemo kufukuzwa kazi,kupunguziwa mshahara au kushushwa cheo. Aidha amewataja watumishi hao kuwa ni Thobias Kahindi ,Aloyce Lukas Ngomeni,ambao walikuwa ni Maafisa watendaji wa vijiji wote wawili walipatikana na makosa ya jinai, wengine ni Marko Mwanzalima Afisa Mtendaji wa kijiji,Godson Elisal yeye ni tabibu msaidizi ambao kwa pamoja walikutwa na kosa la utoro kazini. Katika hatua nyingine baraza hilo limetoa onyo kwa Samweli Mgeta ambaye ni Afisa mtendaji wa kijiji,Kanyumi alipohojiwa kuhusu utambuzi wa vituo vyao vya