AFIKISHWA MAHAKAMANI KISA NYAVU HARAMU WILAYANI SENGEREMA

Mtu mmoja amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa tuhuma ya kukutwa na nyavu haramu aina ya timba.

Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Bi Monica Ndyekobora mwendesha mashitaka wa jeshi  la polisi Inspector Slivester Mwaiseje amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Boazi  Jackson  mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa kijiji cha Bulyaheke wilayani Sengerema mkoani humo.

Inspekta Mwaiseje amesema mtuhumiwa ametenda kosa hilo October 23 mwaka huu majira ya saa mbili katika kijiji cha Bulyaheke wilayani Sengerema kinyume na kifungu cha 66 kifungu kidogo cha kwanza  (a) na kifungu kidogo cha 4 cha kanuni za uvuvi cha mwaka 2009 kinachotokana na kifungu cha 57 cha sheria ya uvuvi namba 22 cha mwaka 2003.


Mshitakiwa amekana kosa hilo hivyo amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini na kesi yake itatajwa tena kwa maelezo ya awali novemba 28 mwaka huu mahakamani hapo.
Na NEEMA HUSSEN.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WANAFUNZI WAONDOKANA NA ADHA YA KUTEMBEA UMBALI MREFU KUFUATA ELIMU KATIKA KIJIJI CHA ILEKANILO WILAYANI SENGEREMA.