AFIKISHWA MAHAKAMANI KISA NYAVU HARAMU WILAYANI SENGEREMA
Mtu mmoja amefikishwa
katika mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa tuhuma ya kukutwa na
nyavu haramu aina ya timba.

Mbele ya hakimu mkazi
wa mahakama hiyo Bi Monica Ndyekobora mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Inspector Slivester Mwaiseje
amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Boazi Jackson
mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa kijiji
cha Bulyaheke wilayani Sengerema mkoani humo.
Inspekta
Mwaiseje amesema mtuhumiwa ametenda kosa hilo October 23
mwaka huu majira ya saa mbili katika kijiji cha Bulyaheke wilayani Sengerema
kinyume na kifungu cha 66 kifungu kidogo cha kwanza (a) na kifungu kidogo cha 4 cha kanuni za
uvuvi cha mwaka 2009 kinachotokana na kifungu cha 57 cha sheria ya uvuvi namba
22 cha mwaka 2003.
Mshitakiwa amekana kosa
hilo hivyo amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini na kesi yake itatajwa tena
kwa maelezo ya awali novemba 28 mwaka huu mahakamani hapo.
Na NEEMA HUSSEN.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete