PESA YAWASABABISHA BODABODA KUTOA SADAKA MAISHA YAO WILAYANI SENGEREMA
Waendesha Bodaboda Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuacha kujitoa mhanga kuhatarisha maisha yao kwa kufanya kazi nyakati za usiku. waendesha bodaboda wakifanyakazi nyakati za usiku Tahadhari hiyo imetolewa na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Wilayani Sengerema PC NORSHIRD MUSSA kufuatia baadhi ya waendesha bodaboda kuendelea kukaidi agizo la serikali la kufanya kazi mwisho saa sita usiku. Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa waendesha bodaboda wilaya ya Sengerema Bwn,KANZU SELEMAN na katibu wake JOSEPHAT JOHN wameunga mkono kauli ya jeshi la polisi kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi pamoja na kuhatarisha usalama wao. Licha ya serikali kupiga marufuku waendesha bodaboda kufanya kazi nyakati za usiku ili kulinda usalama wao lakini suala hilo bado linaendelea wilayani Sengerema. Na,Em