UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA WAMFIKISHA MAHAKAMANI WILAYANI SENGEREMA
Mtu
mmoja amefikishwa katika
mahakama ya wilaya
ya Sengerema mkoani
mwanza kwa tuhuma
ya unyangh’anyi wa kutumia
silaha.
Akisoma
shitaka linalomkabili mbele
ya hakimu wa
mahakama hiyo BI
MONIKA NDYEKOBORA ,mwendesha
mashitaka wa jeshi
la polisi INSPECTA
MARTHA SLIVESTA ,amemtaja
mshitakiwa kuwa ni ISACKA
GELARDI mwenye umri
wa miaka 28 mkazi
wa KATWE wilayani
hapa.
INSPECTA
MARTHA amesema kuwa
mshitakiwa anashitakiwa kwa
kosa la tuhuma ya unyangh’anyi
wa kutumia silaha kinyume
na kifungu namba 287 A cha
kanuni ya adhabu
sura ya 16,
kuwa mnamo januari 18 mwaka huu
majira ya saa 8:00 usiku huko katika kijiji
cha katwe wilayani
sengerema mkoani mwanza aliiba
pesa tathilimu shilingi
elfu hamsini simu
1 aina ya Aitel yenye
thamani ya shilingi
elfu ishilini na
nne na jumla
ya mali yote
ni shilingi elfu
sabini na nne
mali ya NDALO
SAGATI.
Hata
hivyo mshitakiwa amekana
kutenda kosa hilo
na mshitakiwa amerudishwa rumande
kwa hadi
februari 15 mwaka
huu kesi hiyo
itatajwa kwa maelezo
ya awali mahakamani
hapo.
Na Joyce Rollingstone.

Comments
Post a Comment