WAZAZI WAMEWEKA MIKAKATI YA KUDHIBITI UTORO WA WANAFUNZI SHULENI WILAYANI SENGEREMA
Wananchi
wa Kijiji cha Kijuka
kata ya Nyamazugo wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameweka mikakati
ya kudhibiti utoro wa wanafunzi
shuleni ikiwa ni pamoja na kuwachukulia
hatua kali wazazi ambao watoto wao hawatahudhuria shuleni.
Hayo
yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha kijuka Bw, Sospeter Lusapa Dotto
alipoongea na Radio Sengerema ofisini kwake.
Mwenyekiti
amewataka wazazi kutowazuia watoto kwenda shule na kuwaomba kutoa ushirikiano
ili kuhakikisha wanafunzi wanatumia vyema fursa ya serikali ya elimu bure na
kuinua kiwango cha ufaulu.
Aidha
amebainisha changamoto ya upungufu wa madawati iliyopo shuleni hapo na
kuwataka wananchi kuweka utaribu wa kuchangia ili kumaliza kero hiyo.
Mwenyekiti amewataka wazazi na walezi kuwa makini na
watoto ili kuwajengea uwezo na ufaulu mzuri pasipokuwa na visingizio vya utoro
kitendo ambacho kinadidimisha kiwango cha elimu shuleni hapo .

Comments
Post a Comment