WANAHABARI NCHINI WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI NA WELEDI WA TAALUMA YAO
Waandishi
wa habari nchini wametakiwa kuzingatia maadili na weledi wa taaluma yao katika
utendaji kazi ili kukuza taaluma.
Hayo
yamesemwa na mkufunzi wa mafunzo yakuandika habari kwa waandishi wa habari za
vijijini BI ROSE HAJI MWALIMU yanayoendelea katika Ukumbi wa Wakala Wa Majengo
mkoani DODOMA.
Amesema
waandishi wa habari wanatakiwa kutokwenda kinyume na maadili kwa kuandika
taarifa za ukweli, pamoja na kutumia vyanzo vinavyoaminika kwa kuzingatia
kanuni na taratibu za uandishi wa habari.
Akichangia
mada hiyo mmoja wa washiriki katika warsha hiyo MATHIAS TOOKO amesema endapo
waandishi wa habari watazingatia waliyofundishwa wataleta ufanisi na kuongeza uaminifu na mvuto kwa
wasikilizaji.
Mafunzo
hayo ya siku nane yanayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni –UNESCO- yatahitimishwa tarehe 13 mwezi wa pili kwa maadhimisho Siku
ya Redio Duniani.


Comments
Post a Comment