WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA WALALAMIKIA KUTOPEWA DAWA YA KUNYUNYUZIA ZAO HILO MKOANI GEITA
Zaidi ya wakulima 300 wa zao la Pamba katika kijiji cha Ndelema Kata ya
Kamena
Mkoani Geita wameandamana
hadi kwenye ofisi ya afisa mtendaji wa kijiji hicho wakilalamikia
kutopewa dawa ya kunyunyuzia Pamba inayokidhi
mahitaji ya wakulima.

Maandamano hayo ya wakulima yamekuja kutokana na
bodi ya Pamba kuwaletea chupa
35 pekee za dawa ili hali wakulima
wa zao hilo wako zaidi ya 300 katika kijiji hicho ,huku mazao yao yakiendelea kushambulia
na wadudu shambani.
Naye
Mhasibu wa Kijiji
hicho Bwn. Malimi Lushinge katika
hali ya kushangaza amewambia wakulima
hao hajui ni lini
bodi ya pamba itawaletea dawa
hizo , huku akilazimika kuwaonyesha
stakabadhi ya chupa 35 za
dawa zilizopo.
Kwa upande
wake Afisa Mtendaji wa kijiji
hicho
Bwn, John Kahindi amesema kuwa
mamalamiko ya wakulima hao ni ya
msingi kwa kuwa dawa iliyoletwa haikidhi mahitaji ya wakulima na kuweka wazi kuwa tayari amawasiliana na afisa kilimo ngazi ya kata
ili
kupata ufumbuzi wa
tatizo hilo.
Maandamano
ya Wakulima wa pamba
katika kijiji cha Ndelema kulalamikia
kupewa dawa ya kunyunyizia zao la
pamba yamesababisha wasitishe shughuli
zao kwa kwa siku nzima.
Na Emmanuel Twimanye.
Comments
Post a Comment