SERIKALI YAWAONDOA HOFU WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA SENGEREMA JUU YA UPATIKANAJI WA DAWA
Kutokana na Wakulima wa zao la Pamba wilayani Sengerema
kufanikiwa kuvuka lengo la kulima zao hilo Serikali
imewaondoa wasiwasi kuhusiana na
upatikanaji wa dawa.
Akizungumza na Radio
Sengerema Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh.Emmanuel Kipole amesema kuwa,wananchi
wameonesha mwitikio mkubwa baada ya kuhamasishwa na serikali ,hali iliyopelekea wavuke lengo kutoka hekari
elfu 28 walizotarajia zilimwe hadi kufikia ekari Elfu
44.
Aidha,Mh.Kipole amewaondoa
hofu wakulima kuhusiana na tatizo la uhaba wa dawa na kuahidi kuwa itapatikana,
kwani wanaendelea kufanya jitihada ili kukamilisha upatikanaji wake.
Hata hivyo,wakulima wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya
upatikanaji wa dawa, hali ambayo imezua hofu kubwa miongoni mwa wakulima ikiwemo kuharibiwa kwa kushambuliwa na wadudu mazao
yao katika mashamba yao
Na,MICHAEL MGOZI
Comments
Post a Comment