MOTO MKUBWA WATEKETEZA BWENI LA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI KATUNGURU SENGEREMA
Moto mkubwa umezuka na kuteketeza bweni
la wavulana katika shule ya Sekondari Katunguru iliyopo wilayani Sengerema
mkoani Mwanza huku chanzo chake kikiwa hakifahamiki.
Hayo yamethibitishwa na mkuu wa shule hiyo Mwalimu Baraka Ezekiel
Msimba ambapo amesema moto huo umetekeza vitu vyote vilivyokuwa ndani ya
bweni hilo huku wanafunzi takribani 5 wakinusurika kifo.
Kufuatia ajali hiyo mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ametoa pole kwa wahanga wa tukio
hilo huku akiahidi kuchangia akiahidi kuchangia magodoro 50 mifuko 50 ya
saruji.
Mkuu wa mkoa ameagiza kuanza ujenzi wa mabweni hayo mara moja.
Nao wanafunzi wameeleza kwa masikitiko makubwa huku wakidai kuwa ajali hiyo hawajui imetokana na nini kwani wao walikuwa darasani wakijisomea.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Sengerema amewataka wanafunzi kusoma
kwa bidii licha ya kukumbwa na ajali hiyo.









Comments
Post a Comment