MKUTANO WA KIJIJI WASABABISHA KUSIMAMA KWA SHUGHULI ZA UCHENJUAJI WA MADINI YA DHAHABU MKOANI GEITA
Mkutano wa serikali ya Kijiji cha Mawemeru kata ya Nyarugusu
wilayani Geita,umezuia shughuli za uchenjuaji wa Madini ya Dhahabu zinazofanywa
na Mgodi wa Plas uliopo katika Kitongoji cha Mgombani,kutokana na Mgodi huo
kuwa kwenye makazi ya watu.

Mkutano huo wa dharula umekutana baada ya Kupokea Malalamiko ya
Wananchi wanaoishi jrani na Mgodi huo wakihofia maisha yao kutokana na kemikali
zinazotumika kuchataka madini hayo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mawemeru
Mlindwa Maganga akatoa Ufafanuzi na
baadaye Kaimu Mtendaji akasoma Taarifa ya wakazi wa Kitongoji cha Mgombani.
Wakazi wa Kitongoji cha Mgombani wahofia Maisha yao hasa kwa
watoto wao kutokana na Uwepo wa Mgodi huo,kwani sumu inayotumika ni hatari kwa
viumbe hai.
Mwenyekiiti wa Wafugaji
kata ya Nyarugusu Selestine Hechimubi amesema Shughuli hizo zinahatarisha
Viumbe hai Vingine wakiwemo mifugo.
Aidha,Diwani wa Kata ya Nyarugusu Swalehe Juma amebariki maamzi ya
Mkutano huo na kumtaka Mwekezaji kama hakuridhia uamzi huo kukata rufaa ngazi
nyingine.
Meneja wa Mgodi huo Aulice Mtegeta amesema Uongozi wa Mgodi
umepokea kwa masikitiko Makubwa maamzi ya Mkutano huo.
Comments
Post a Comment