MIMBA ZA UTOTONI ZABISHA HODI WILAYANI SENGEREMA


Wazazi  wa  kijiji  cha  Tunyenye  kata  ya  Kishinda  wilayani Sengerema wametakiwa kuzingatia  malezi   kwa  watoto  wa  kike hususani   walioko  mashuleni    ili  kujiepusha na wimbi  kubwa  la mimba  za  utotoni.   




Hayo yamebainishwa na  Afisa mtendaji wa kijiji cha Tunyenye bwn Samson Peleka  wakati akiongea na  Radio Sengerema amesema hayo baada  ya  wanafunzi  2  wa shule ya msingi na secondari   Tunyenye kupatiwa ujauzito    

Kwa hatua nyingine Peleka amewataka wanafunzi kuepuka vishawishi na kuacha tabia ya  kujiunga  na makundi mabaya kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Na,  BWIZA BONIPAHACE 

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WANAFUNZI WAONDOKANA NA ADHA YA KUTEMBEA UMBALI MREFU KUFUATA ELIMU KATIKA KIJIJI CHA ILEKANILO WILAYANI SENGEREMA.