MBUNGE WA JIMBO LA SENGEREMA AKABIDHI MIFUKO 200 YA SARUJI KATIKA SHULE YA SEKONDARI KATUNGURU

Moto mkubwa uliozuka na kuteketeza bweni la wavulana katika shule ya Sekondari
Katunguru iliyopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza usiku wa kuamkia februari 07
mwaka huku chanzo chake kikiwa hakifahamiki hatimaye Mbunge wa Jimbo la
Sengerema Mh William Mganga Ngeleja akiwakilishwa na Diwani wa Kata ya
Katunguru Mh Methew Lubongeja amekabidhi mifuko 200 ya saruji.
![]() |
| Diwani wa Kata ya Katunguru Mh,Methew Lubongeja (Kushoto) akikabidhi mifuko 200 ya Saruji kwa mkuu wa shule ya Sekondari Katunguru Mwalimu Baraka Ezekiel Msimba (kulia) |
Diwani Mathew Lubongeja akiongea na jumuiya ya wanafunzi wa Katunguru Sekondari baada ya kukabidhi mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na Mh mbunge William Mganga Ngeleja kwa ajili ya ujenzi mpya wa bweni lilioungua na moto .

Diwani Mathew Lubongeja amemuwakilisha mh William Ngeleja kutoa mifuko ya saruji 200 kuchangia kujenga bweni jipya baada ya bweni la awali kuungua moto katika Shule ya Sekondari Katunguru,
Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Baraka Ezekiel Msimba amemshukuru mh Mbunge wa Jimbo la Sengerema kwa msaada alioutoa kwa wakati huu mgumu wa
majonzi.
Na Veronica Martine.

Comments
Post a Comment